Friday , 24 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni
Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Dk. Peter Mathuki
Spread the love

Aliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter Mathuki anatarajiwa kuhojiwa na Kamati  ya sheria, Haki, na Hadhi ya Bunge la Jumuiya  hiyo juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka,ofisi na mali za Jumuiya. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Dk. Mathuki ambaye aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo Mei 2021 na serikali ya nchi yake ya Kenya, alitenguliwa na kupangiwa kazi nyingne na rais wa nchi hiyo Aprili mwaka 2024 baada ya baadhi ya wabunge kuwasilisha tuhuma zake katika kikao cha bunge hilo kilichokuwa kimekaa Nairobi nchini Kenya.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabili Dk. Mathuki ni zile zinazohusishwa na matumizi mabaya ya ofisi, madaraka na mali za Jumuiya hiyo.

Tuhuma hizo zimefikishwa rasmi kwenye kamati ya sheria, haki na hadhi ya bunge hilo ambayo mwenyekiti wake Mashaka Ngole kutoka Tanzania amesema imeanza kuzifanyia kazi.

“Leo kama kamati tumekutana kwa lengo la kupata picha halisi kwamba hizo tuhuma uthibitisho wake uko wapi na kamati imepokea tuhuma kama zilivyowasilishwa na mpaka sasa hivi kamati haiwezi kusema lolote.

“Lakini tuhuma ni nyingi na ukizitazama zinazungumzia matumizi mabaya ya ofisi, masuala ya fedha, mambo ya uajiri ni mambo mengi yametajwa ambayo yanatuhitaji kutumia muda mwingi kuyapitia kwa kina,” amesema.

Kwa mujibu wa Ngole katika utekelezaji wa majukumu hayo kamati inatarajia kuwashirikisha watu wote waliotajwa kushiriki katika mtandao huo akiwemo mtuhumiwa mwenyewe Dk. Mathuki

Kwa kuwa ofisi zote zilizotajwa zina watu hivyo kamati italazimika kuwaita na kuwasikiliza juu ya hayo mambo yote yaliyotajwa kufanyika kwenye ofisi zao.

 

“Kwa hiyo wao ndio watatusaidia kutupatia ukweli halisi lakini tukimaliza hilo tutamuita pia mtuhumiwa Dk. Mathuki ili naye tumsikie,” amesema.

Tuhuma dhidi ya katibu mkuu huyo ziliibuliwa na mbunge wa bunge hilo kutoka Sudan kusini, Kenned Mukulia ambaye pia amesema tatizo ni kubwa zaidi ya linavyoonekana na kwamba upo mtandao mkubwa na ushahidi kwenye ripoti iliyowasilishwa kwenye kamati.

“Hili sio suala la katibu mkuu peke yake kuna watu wengine wengi wameshiriki kuwezesha na kufanikisha haya mambo yaani ni mtandao mkubwa,” alisema mbunge huyo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kamati hiyo pamoja na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ofisi na mali za Jumuiya Dk. Mathuki ambaye kwa sasa serikali ya Kenya imemteua kuwa balozi pia anatuhumiwa kukiuka sheria za ajira za wafanyakazi na kwamba kamati hiyo baada ya kumaliza kazi yake itakabidhi ripoti kwenye Bunge la Jumuiya hiyo.

Licha ya baada ya Rais wa Kenya, William Rutto kumuondoa Dk. Mathuki na kuteua Katibu mkuu mwingine hadi sasa bado hajaanza kazi na pia hajathibitishwa na ngazi zinazohusika ikiwemo ya wakuu wa nchi kama taratibu zinavyoelekeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo

Spread the loveRAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 63 ya Uhuru bila katiba ya wananchi

Spread the loveWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanaharakati...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Serikali mbili ni sera ya CCM, si mkataba wa Muungano

Spread the loveMUUNGANO kati ya Tanganyika na Zanzibar uliotimiza miaka 60 tangu...

error: Content is protected !!