Friday , 24 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo
Habari za Siasa

CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimejipanga kujijenga kisiasa kuelekea chaguzi zijazo kwa kufanya mikutano mikubwa ya hadhara pamoja na kueneza sera zake nchi nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mipango hiyo imetajwa na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umm CUF, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, leo tarehe 14 Mei 2024.

Taarifa ya Mhandisi Ngulangwa imesema, tarehe 25 hadi 29, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, atafanya ziara wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, ambapo atafanya mkutano mkubwa wa hadhara.

“CUF kimepanga kuivuruga Tanzania nzima kwa mfululizo wa matukio ya mikutano mikubwa ya hadhara na harakati za Uenezi zitakazoambatana na mapokezi ya mamia ya wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali na wasio wanachama wa chama chochote,” imesema taarifa ya Mhandisi Ngulangwa.

Katika hatua nyingine, taarifa ya Mhandisi Ngulangwa imesema tarehe 27 na 28 kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa CUF,  kitafanyika ambapo kinatarajiwa kupitisha majina ya wagombea nafasi za uenyekiti wa chama hicho ngazi ya wilaya na wajumbe wa mkutano mkuu Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo

Spread the loveRAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 63 ya Uhuru bila katiba ya wananchi

Spread the loveWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanaharakati...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Serikali mbili ni sera ya CCM, si mkataba wa Muungano

Spread the loveMUUNGANO kati ya Tanganyika na Zanzibar uliotimiza miaka 60 tangu...

error: Content is protected !!