Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Nape atangaza ujio mkakati mpya wa upashanaji habari serikali
Habari Mchanganyiko

Nape atangaza ujio mkakati mpya wa upashanaji habari serikali

Spread the love

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema wizara hiyo ipo hatua ya mwisho ya kukamilisha utayarishaji wa mkakati wa Taifa wa mawasiliano kwa umma ambao utarahisisha upatikanaji na usambambazaji wa taarifa za serikali kwa umma. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ…(endelea).

Amesema hayo leo tarehe 27 Machi 2023 katika kikao cha 18 cha maafisa habari na mawasiliano wa serikali, Dar es saalam ambacho kimefunguliwa na Waziri Mkuu Tanzania, Kassim Majaliwa.

                                                                                Nape amesema mradi huo utakapokamilika na kuanza kutumika, utaleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya habari nchini pamoja na sekta nyingine.

“Mradi huu utaweka misingi ya kusimamia usambazaji wa taarifa zenye maudhui ya ajenda za kitaifa, utaweka na kuboresha mbinu na teknolojia ya ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa taarifa za serikali kwa wananchi,” amesema Nape.

Pia amesema utaweka mfumo madhubuti wa namna serikali inavyopaswa kutoa ufafanuzi, kukanusha, kutuliza na kutoa hofu wananchi pale ambapo kutatokea mkanganyiko au taarifa za upotoshaji.

Sambamba na hilo amesema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kisasa kwa baadhi ya vitengo vya habari katika wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali na upungufu wa maafisa habari kwa baadhi ya maeneo wa serikali.

Waziri Nape pia amependekeza mambo ambayo yataweza kukabiliana na changamoto hizo ambazo wizara yake inakabiliana nazo kuwahuisha miundo ya kada ya maafisa habari serikalini na kuongeza idadi ya ajira kwa maafisa habari serikalini.

“Kuhimiza wizara, mamlaka za serikali za mitaa, tawala za mikoa, wakala idara za serikali zinazojitegemea, taasisi nyingine za Umma kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya shughuli za habari na mawasiliano kwa Umma,” amesema hayo Nape.

Mwisho ametoa tuzo kwa waziri mkuu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika mchango alioutoa kwa sekta hiyo ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!