Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sungusia: Nataka kuikwamua TLS
Habari Mchanganyiko

Sungusia: Nataka kuikwamua TLS

Wakili Msomi Harold Sungusia
Spread the love

MGOMBEA Urais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Wakili Harold Sungusia, amesema  malengo yake ni kukikwamua chama hicho ili kiweze kutoa mchango wake kwenye maendeleo ya utawala wa sheria nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wakili Sungusia ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Machi 2023, akizungumza na MwanaHALISI Online, juu ya sababu zilizomsukuma kugombea Urais wa TLS, katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.

“Naamini nikiungana na mawakili wenzangu tunaweza kuikwamua TLS hapo ilipo na kuwezesha kutoa mchango kwenye maendeleo ya utawala wa sheria Katika nchi yetu,” amesema Sungusia.

Katika hatua nyingine, Wakili Sungusia amesema TLS inahitsji uongozi utakaojenga mifumo inayolinda na kuboresha maslahi ya mawakili, na kwamba amejitathmini na kuona anatosha kufanikisha lengo hilo.

Akitaja vipaumbele vyake, Wakili Sungusia amesema akifanikiwa kushinda Urais wa TLS atahakikisha mazingira ya biashara ya mawakili yanaboreshwa, ikiwemo kwa kuondoa vishoka, michango isiyo na tija, kuondoa tatizo la utoaji malipo madogo ya hufuma za mawakili kinyumr Cha sheria.

Vipaumbele vingine ni kuhakikisha mawakili wanapata huduma bora za afya au matunzo watakapozeeka, mawakili vijana wanapata mitaji ili kuanzisha ofisi zao baada ya kumaliza masomo.

“Kuna mambo ambayo TLS ingeweza kuyatatua ili kuboresha mazingira ya biashara ya mawakili, kama kuondoa tatizo la vishoka, kuondoa michango ambayo ni kero kwa mawakili.hasa vijana kama mchango wa lazims kwa uanachama wa East African Law Society,” amesema Sungusia na kuongeza:

“Nikifanikiwa kuwa Rais, nitaondoa changamoto ya kutoheshimika kwa mihuri ya mawakili, ofisi za mikoa kukosa fedha na kupungua kwa miradi ya maendeleo kunakosanabisha  TLS iwe tegemezi kwa michango ya mawakili.”

Katika uchaguzi huo, Wakili Sungusia atachuana na Wakili Reginald Shirima, ambaye wamejitosa kuwania nafasi ya urais wa TLS, inayoshikiliwa na Prof. Edward Hosea, anayemaliza muda wake. Mwingine aliyejitosa katika kinyang’anyiro hicho ni Sweetbeart Nkuba, ambaye amekata rufaa kupinga jina lake kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TLS.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

error: Content is protected !!