May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Namungo FC yakwama Uwanja wa ndege Angola

Kikosi cha timu ya Namungo FC

Spread the love

 

MSAFARA wa wachezaji na viongozi wa klabu ya Namungo FC umezuiliwa katika Uwanja wa ndege wa Luanda nchini Angola kwa madai kuwa wachezaji wao watatu na kiongozi mmoja wana maambukizi ya virusi vya corona. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kuzuiwa huku kwa klabu hiyo ni baada ya malmaka ya Uwanja huo kutaka msafara mzima wa klabu hiyo kurudi Tanzania au kukaa karantini.

Namungo imesafiri nchini humo kwa ajili ya kucheza mchezo wa raundi ya tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Desportivo 1 de Agosto kwa mechi ya mzunguko wa kwanza.

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa siku ya kesho tarehe 14 Februari 2021, kwenye dimba la Franca Ndalu uliopo kwenye mji wa Luanda nchini humo.

Mpaka inafika nchini humo Namungo FC iliondoka na jumla ya wachezaji 22.

error: Content is protected !!