Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu My Legacy yagusa shule 28 Kinondoni
Elimu

My Legacy yagusa shule 28 Kinondoni

Spread the love

 

MRADI unaohamasisha utunzaji wa mazingira na hedhi salama ( Wash), unaotekelezwa na Taasisi ya Urithi Wangu (My Legacy), umegusa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari 28 za Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa huyo imetolewa leo tarehe 28 Oktoba 2023 na Mratibu wa Program na utafutaji rasilimali wa My Legacy, Amina Ally, katika warsha ya siku moja ya wadau wa elimu na serikali kwa ajili ya kupena mrejesho wa mradi huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amina amesema mradi huo umegusa moja kwa moja wanafunzi 1,000, waliopewa mafunzo ya elimu ya hedhi salama, usafi wa hedhi, haki zao na namna ya kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kutengeneza sodo za kufua (pedi), ambao watakuwa mabalozi katika kuwafikia wanafunzi wengine zaidi ya 40,000.

Mratibu huyo wa My Legacy, amesema kupitia mradi huo wamefanikiwa kujenga vyoo maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujihifadhi wakati wa hedhi, katika shule tano wilayani humo.

Pia, Amina amesemamradi huo umegusa walimu 30 ambao wamepewa elimu juu ya uingizaji afua za mradi huo wakati wanafundisha wanafunzi.

“Mbali na masuala ya hedhi salama na usafi wa mazingira, mradi hjuu unaendelea na uchechemuzi wa haki za wnaawake na vijana katika masuala ya rasilimali ardhi. Matokeo ya mradi huu ni mazuri na wanafunzi 1,000 waliopewa mafunzo tuanatarjia watawafikia watu wengine 40,000 kupitia elimu rika,” amesema Amina.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu ya Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Kinondoni, Mwanaisha Maulid, amesema serikali itaendelea kushirikiana na My Legacy ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ukamilifu.

Mwakilishi mkazi wa Shirika linalohusiana na makazi, (Habitat for Humanity), Fortunata Temu, amesema “ushauri wangu kwa watekelezaji na wanufaika, hasa jamii inatakiwa iendeleze yaliyoanzishwa kama tunavyojua mradi ni muda mfupi na ikifika ukomo haimaanishwi kilichotekelezwa kinaishia hapo, wana jamii wnaapswa kuendeleza ili kuleta matokeo endelevu.”

Wakizungumza katika warsha hiyo, baadhi ya walimu ambao ni wasimamizi wa mradi wa Wash katika shule zao, wamesema mradi huo umesaidia kutatua changamoto mbalimbali za wanafunzi ikiwemo usafi waazingira na hedhi salama.

Wamesema mradi huo umesaidia wanafunzi kupata maji baada ya mradi huo kuwapatia matanki ya maji. Pia, umesaidia wanafunzi kujifunza stadi za maisha ikiwemo utengenezaji wa sabuni, bustani za maua na mbogamboga na vifaa vya kufundishia.

Kuhusu hedhi salama, walimu wamesema mradi wa Wash umesaidia kuwajengea uelewa wanafunzi wa kike juu ya suala hilo na namna ya kulinda afya wanapokuwa katika siku zao, pamoja na kutengeneza sodo (Pedi) za kufua, ili kuokoa gharama.

Mwalimu kutoka Shule ya Msingi Nakasangwe, Sarah Daffa, amesema wanafunzi zaidi ya 70 na walimu 10 wamenufaika Moja Kwa Moja na mradi huo kwa kupata Mafunzo mbalimbali ambao wamekuwa mabalozi wa kusambaza Elimu hizo kwa wengine.

“Shule yetu imenufaika na mradi wa Wash, kwanza sabuni zinazotengenezwa zinatumika shuleni na kuokoa gharama za kununua sabuni mara kwa mara. Pia, wanafunzi wamenufaika na elimu ya kunawa mikono mara kwa mara kitendo iinachowaupusha na magonjwa,” amesema Daffa.

Naye Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mivumoni, Hilda Sanga amesema “kupitia mradi huu tumefanikiwa kutoa elimu ya usafi wa mazingira na afya, tumewafundisha wanafunzi kutengeneza sodo na sabuni. Wanafunzi 57 n walimu 10 wamenufaika na mradi huu.”

Kwa upande wake Mwalimu wa Shule ya Msingi Mirambo, Agness Sinzobakwila, amesema kupitia mradi wa Wash wamefanikiwa kutunza mazingira ya shule kwa kutengeneza bustani, kupanda miti, pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama Kwa wanafunzi.

Mwalimu kutoka Shule ya Msingi Lugalo, Hassan Mirimo, amesema kupitia mradi huo wamefanikiwa kupanda miti, kufanya usafi pamoja na wanafunzi kupata maji ya uhakika kutokana na My Legacy kuwapa matenki ya maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!