Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwenge warejesha Bil. 2.2/- za mfuko wa maendeleo ya vijana
Habari za SiasaTangulizi

Mwenge warejesha Bil. 2.2/- za mfuko wa maendeleo ya vijana

Spread the love

MWENGE wa Uhuru wa mwaka 2022 imefanikiwa kurejesha Sh 2.2 bilioni za mfuko wa maendeleo ya vijana ambazo zilikuwa zimekusanywa na Halmashauri na kupelekwa kwenya matumizi mengine tofauti na yaliyokusudiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, tarehe 14, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof, Joyce Ndalichako, katika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge, Kumbukizi ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana zinazofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Ndalichako amesema ukaguzi uliofanywa na timu ya Mwenge wa Uhuru ikishirikiana na vyombo ya uchunguzi imebaini kuwa vijana wanafanya marejesho ya fedha za mikopo lakini hazirudhishwi kwenye mfuko mkuu wa maendeleo ya vijana kwaajili ya kuendelea kukopesha wengine.

Akifafanua zaidi wakati akisoma taarifa ya mbio za Mwenge, Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2022, Said Geraruma amesema pamoja na jitihada za Serikali kuwezesha mfuko huo, fedha hizo zimekuwa zikipotelea kwenye Halmashauri.

“Fedha hizo zimekuwa zikirejeshwa vizuri na vijana katika mfuko wa maendeleo ya vijana lakini cha kushangaza halmashauri zetu zimekuwa zikielekeza fedha hizi kwenye matumizi mengine,” amesema.

Geraruma amebainisha pia kuwa Halmashauri nyingi hazifuatilii kabisa marejesho ya fedha hali inayodhoofiisha mfuko huo.

“Kwasababu zilizotajwa marejesho yamekuwa hafifu na mifuko ya akaunti na ukaguzi haikufanikiwa kurejesha fedha hizo lakini Mwenge wa uhuru umefanikiwa kurejesha fedha hizo ambapo Sh 2.2 Bilioni zimefanikiwa kurejshwa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!