Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Halmashauri 43 zenye miradi yenye kasoro zaanikwa
Habari za Siasa

Halmashauri 43 zenye miradi yenye kasoro zaanikwa

Prof. Joyce Ndalichako
Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, ameziweka hadharani Halmashauri 43 ambazo zimekutwa na kasoro katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Waziri huyo amesema miradi hiyo imebainika wakati wa ukaguzi uliofanywa na timu ya mbio za Mwenge za mwaka 2022.

Ndalichako amebainisha hayo leo Ijumaa tarehe 14 Oktoba, 2022, katika kilele cha mbio za mwenge, kumbukizi ya Baba wa Taifa, na Wiki ya Vijana inayofanyika mkoani Kagera.

Amesema halmashauri hizo zinajumuisha Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya zenye mkradi yenye kasoro ni pamoja na Mbinga, Mwanging’ombe, Tandaimba, Newala, Tandaimba, Nanyamba, Mtwara, Mtama Liwale, Kilwa Rufuji Kibiti Mkuranga, Kisarawe Mkinga.

Zingine ni Halmashauri za Wilaya ya Pangani, Kilindi Handeni, Lushoto, Same, Mwanga, Rombo, Moshi, Simanjiro, Mbulu, Karatu, Monduli, Serengeti, Busega, Bariadi, Meatu, Geita, Malinyi na Wilaya ya Kaskazini B Kusini Unguja.

Kwa upande wa Halmashauri za miji, Nadlichako amebainisha kuwa ni Mtwara, Babati, Mbulu na Bunda huku Halmashauri za Manispaa ni Songea, Kinondoni Ubungo na Temeke na Halmashauri ya jiji ni Ilala na Tanga.

“Kwa miradi ambayo ilikutwa na lasoro ndogo maelekezo yalitolewa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufuatilia na kuhakikisha zinaondolewa ili wananchi waweze kupata huduma zinazostahili,” amesema Ndalichako.

Akisoma taarifa ya miradi yenye dosari na taarifa ya awali ya TAKUKURU, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa mwaka 2022, Said Geraruma, ameweka wazi kasoro zilizobainika katika miradi mingi ni pamoja na miradi kujengwa kinyume na mikataba, kufanya malipo kwa mkandarasi bila kuwepo kwa hati ya kuthibitisha kukamilika kwa kazi, kutokuwepo malipo ya kodi ya zuio ya mradi , matumizi ya vifaa duni ikiwemo mbao, gypsum, vitasa, bawaba, aluminium, bomba, marumaru nondo na vyuma vyenye ujazo mdogo tofauti na maelekezo ya wataalamu.

“Matatizo haya ndiyo chanzo cha kuwa na miradi isiyo na ubora wakati malipo yanafanyika kama ilivyo katika BOQ,” amesema Geraruma.

Ameongeza kuwa wakandarasi wa miradi hawasimamiwi ipasavyo na wahandisi wa Halmashauri na hivyo kutekeleza miradi chini ya kiwango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!