Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwendesha mashtaka mauaji ya Rais wa Haiti aachishwa kazi
Kimataifa

Mwendesha mashtaka mauaji ya Rais wa Haiti aachishwa kazi

Bed-Ford Claude
Spread the love

 

ARIEL Henry, waziri mkuu wa Haiti, amemfuta kazi mwendesha mashItaka mkuu wa taifa hilo, Bed-Ford Claude, kufuatia uamuzi wake wa kutaka kumfungulia mashitaka ya mauaji ya Rais Jovenel Moise. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uamuzi wa waziri huyo mkuu, umetajwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Haiti, kwamba unaweza kuitumbukiza Haiti katika mzozo mpya wa kisiasa.

Nafasi ya Claude imechukuliwa na Frantz Louis Juste, mwendesha mashitaka aliyesimamia kesi iliyohusisha vifo vya zaidi ya watoto 12 walioteketea katika kituo cha watoto yatima mjini Port-au-Prince mwaka jana.

Wiki iliyopita, Bed-Ford Claude – aliyekuwa mwendesha mashitaka katika kesi hiyo –  alisema, rekodi za simu zinaonyesha kuwa mtu anayeshukiwa kuwa mpangaji mkuu wa mauaji ya Moise, aliwasiliana na Waziri Mkuu Henry usiku ambao uhalifu huo ulifanyika.

Anasema, waziri mkuu na mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa majina ya Joseph Baido, kwa sasa, hajulikani alipo. Mwendesha mashitaka anasema, Baido na waziri mkuu Henry, walizungumza mara mbili kwa kipindi cha dakika saba kila mara.

Baido alikuwa afisa katika wizara ya sheria na ambaye Henry amekuwa akimtetea, anadaiwa kutoroka na hajulikani alipo.

“Vitendo vya kuleta mkanganyiko na kuzuia haki haviwezi kukubalika. Wahusika wa kweli na waliopanga mauaji ya Rais Moise watafunguliwa mashitaka na wataadhibiwa kwa vitendo vyao hivyo,” alieleza waziri mkuu Henry.

Henry, ambaye ni daktari wa upasuaji aliteuliwa na Moise kushika wadhifa wa waziri mkuu siku chache kabla kuuwawa kwake na anajinasibu kutaka kuleta maelewano kati ya mirengo mbalimbali ya kisiasa.

Hata hivyo, kuibuka kwa madai yanayomhusisha na mauaji ya Rais Moise, yananifunika adhima yake ya kuleta maelewano ya kisiasa nchini mwake.

Haijawa wazi iwapo kuondolewa kwa Claude kutakuwa na athari yoyote katika kesi hiyo ila wachambuzi nchini humo wanasema, hawatarajii mengi kuhusiana na kesi hiyo kubadilika kwasababu uchunguzi upo mikoni mwa jaji.

Hapo Jumatatu, Waziri wa sheria nchini humo Rockfeller Vincent aliiagiza polisi ya Haiti kumuongezea ulinzi Claude kwasababu alikuwa amepokea vitisho kwa kipindi cha siku tano.

Fauka ya hayo, makarani wa korti wanaripotiwa kwenda mafichoni baada ya kupokea vitisho vya kuuwawa iwapo hawatobadilisha baadhi ya majina na taarifa katika ripoti zao. Mbali na hayo, jaji mmoja aliyepewa jukumu la kusimamia uchunguzi katika kesi hiyo alijiuzulu mwezi uliopita kwa kile alichosema ni sababu za kibinafsi lakini mmoja wa wasaidizi wake alifariki kwa njia ya utata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!