Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi ndogo ya Mbowe: Jamhuri kutumia mashahidi 7
Habari za Siasa

Kesi ndogo ya Mbowe: Jamhuri kutumia mashahidi 7

Spread the love

 

UPANDE wa Jamhuri, katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtama ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, katika Mahakama  Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujunu Uchumi, umedai utatumia mashahidi saba kwenye shauri dogo la kesi hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo namba 16/2021 ni Halfan  Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 15 Septemba 2021 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando mbele ya Jaji Mustapha Siyani, wakati shauri hilo lilipoanza kusikilizwa.

Wakili Kidando amedai shahidi wa kwanza ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Arusha, Ramadhani Kingai, ambaye sasa ni Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar ea Salaam.

Kwa sasa Kamanda Kingai anaendelea kutoa ushidi wake katika shauri hilo, akiongozwa na Wakili Kidando.

Shauri hilo linasikilizwa baada ya mawakili wa Mbowe na wenzake, wakiongozwa na Peter Kibatala,  kuweka mapingamizi mawili dhidi ya maelezo ya mshtakiwa Adam Kasekwa.

Mapingamizi hayo yaliwekwa baada ya Kamanda Kingai hapo awali kutoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya msingi, ambapo alidai alichukua maelezo ya Kasekwa kwa hiari yake.

Mbele ya mahakama hiyo, Kibatala alitoa hoja za mapingamizi hayo, ikiwemo iliyodai kwamba mshtakiwa huyo alichukuliwa maelezo nje ya muda, kinyume cha kifungu cha 50 (1) sehemu A na B pamoja na kifungu  cha 51 na 52 cha Sheria ya Mwenendo wa  Makosa ya Jinai, vinavyoelekeza mtuhumiwa kuchukuliwa maelezo ndani ya saa nne baada ya kukamatwa.

Kibatala alidai kuwa, maelezo hayo ni kinyume cha sheria kwa madai, mshtakiwa huyo alikamatwa tarehe 5 Agosti 2020 mkoani Kilimanjaro na kuhojiwa tarehe 7 Agosti 2020, Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Katika hoja ya pili, Kibatala alidai mshtakiwa huyo alichukuliwa maelezo hayo baada ya kuteswa.

Kufuatia hoja hizo, Wakili Kibatala aliiomba mahakama hiyo mbele ya Jaji Siyani, ifanye shauri dogo ndani ya kesi hiyo, ili mapingamizi yao yatolewe uamuzi.

Nao Mawakili upande wa Jamhuri wakiongozwa na Kidando, walikubali shauri hilo dogo lisikilizwe.

Kufuatia hoja hizo, Jaji Siyani aliridhia ombi hilo na kuanza usikilizwaji wa shauri dogo, ili ipate ushahidi kama mshtakiwa aliteswa wakati anahojiwa au lah.

Endelea kufuatilia MwanaHALIS TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!