September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aahidi kufufua majukwaa yote ya wanawake nchini

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameahidi kukuza uchumi wa wanawake na kutekeleza malengo yote yaliyowekwa na serikali ya wamu ya nne. Anaripoti Patricia Kighono TUDARCo … (endelea).

Rais Samia ameyasema hayo leo tarehe 15 Septemba 2021 katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya demokrasia duniani yaliyofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee

Katika maadhimisho hayo Rais Samia ameahidi kukuza uchumi wa wanawake na kusema anajipanga kuyalea majukwaa mbalimbali ya wanawake na kuwasihi wanawake kuyaendeleza majukwaa hayo na kufufua yale yaliyokufa.

Raisi Samia pia amesisitiza kuendelea kufanyia kazi malengo yote yaliyowekwa na serikali ikiwemo yale ya awamu ya tano.

Amesema anaendeleza mfumo wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari ambao ulikua ni mpango wa Rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli.

Aidha, katika maadhimisho hayo, wanawake wa Tanzania wamempongeza Rais Samia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya urais na kuwapa hamasa wanawake wengine kushika nafasi za uongozi.

Wanawake hao kupitia kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Ulingo wa Wanawake Tanzania, Anna Abdalah wamemkabidhi  Rais Samia tuzo tatu kama ishara ya pongezi na kuendelea kushirikiana nae katika kuleta maendeleo kwa Taifa.

error: Content is protected !!