Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia apokea ujumbe wa Salva Kiir Dar
Habari za Siasa

Rais Samia apokea ujumbe wa Salva Kiir Dar

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir Mayardit, Balozi Albino Ayuel Aboug. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumatano, tarehe 15 Septemba 2021, Ikulu jijini Dar es Salaa.

Balozi Aboug amesema ujumbe huo pamoja na mambo mengine, Rais Salva Kiir Mayardit ametaka kuimarishwa zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Sudan Kusini.

Amesema Sudan Kusini inaomba kutumia Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yake na pia kununua chakula kutoka Tanzania.

Aidha, Balozi Aboug amesema Sudan Kusini pindi Reli ya Kisasa (SGR) itakapokamilika ingependa kusafirishia bidhaa zake kupitia reli hiyo.

Pia, amesema Sudan Kusini bado inahitaji kupata walimu wa kufundisha lugha ya Kiswahili kuanzia ngazi ya shule za msingi kutoka nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Rais Samia amemuhakikishia mjumbe huyo kuwa Tanzania iko tayari kuendeleza ushirikiano na uhusiano uliopo kwa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kuhusu ombi la kutumia Bandari ya Dar es Salaam, Rais Samia amemuhakikishia mjumbe huyo kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na Sudan Kusini kutumia Bandari ya Dar es Salaam katika kukuza uchumi wa nchi zote mbili.

Taarifa ya mazunguzo hayo imetolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!