Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanandoa afumwa akishiriki ngono na mchepuko kanisani, waumini wasusa..
Kimataifa

Mwanandoa afumwa akishiriki ngono na mchepuko kanisani, waumini wasusa..

Spread the love

 

KUNDI la waumini wa Kanisa la Bungonya lililoko wilayani Kayunga nchini Uganda limesusa kushiriki ibada kanisani hapo baada ya wanandoa wawili kufumaniwa ‘wakipiga mechi’ kwenye madhabahu ya kanisa.

Imedaiwa kuwa Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye ni Mkristo wa Kanisa Katoliki alikuwa akizini na mpenzi wake (mchepuko) ambaye hivi karibuni alitalikiwa na mumewe. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa gazeti la Monitor la nchini Uganda, wawili hao walifumwa wakiwa hawajavaa nguo na mke wa mwanaume huyo ambaye aliyetoa taarifa, ambayo ilisababisha kuvutia umati wa watu.

“Wawili hao walikamatwa huku wakilaaniwa na wakazi hao. Kitambaa cha mwanamke na fulana ya mwanaume vimehifadhiwa katika makazi ya Baraza la Mtaa (LC) kama vielelezo,” alisema Mwenyekiti wa Bugonya LC1 George William Kanda.

Kanda alisema kuwa wawili hao waliingia kanisani hapo kupitia dirishani kwani milango ilikuwa imefungwa.

Kanda aliongeza kuwa baada ya tukio hilo, wahusika walipelekwa ofisini kwake na wakazi wenye hasira lakini baadaye aliwaachia huru baada ya kuwashtaki kwa kosa la uasherati. Mpaka jana Alhamisi, mwanaume huyo inadaiwa alikuwa amejificha.

“Kesi haitaoza. Atajibu dhambi yake wakati wowote atakaporejea,” alisema Kanda.
Waumini kutoka Kanisa la Bungonya nchini Uganda sasa wanataka viongozi wa kanisa kufanya ibada ya utakaso ili kusafisha eneo hilo.

Viongozi hao wa kanisa tangu wakati huo wamewahimiza waumini wao kufunga kwa muda usiojulikana kutokana na tukio hilo ambalo wamelitaja kuwa la “kushtua” na la dhambi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!