Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia amburuza mahakamani Selasini, Diamond Platnumz akitaka wamlipe fidia Sh. 10 Bil
Habari za SiasaTangulizi

Mbatia amburuza mahakamani Selasini, Diamond Platnumz akitaka wamlipe fidia Sh. 10 Bil

Joseph Selasini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi
Spread the love

 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amemfikisha mahakamani Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Selasini na wengine sita, akitaka wamlipe kiasi cha Sh. 10 bilioni kama fidia ya kumchafua kufuatia kumtuhumu kuwa ni fisadi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Selasini, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya madai Na. 59/2023, ni kampuni za vyombo vya habari, ikiwemo Mwananchi Communication Limited, Wasafi media inayomilikiwa na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz).

Vyombo vingine ni Jamhuri Media Limited, inayochapisha gazeti la Jamhuri. Global Publishers na Mhariri wa Gazeti la The Citizens.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo tarehe 7 Julai 2023, Wakili wa Mbatia, Hardson Mchau, amedai kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 11 hadi 12 Julai 2023, katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mussa Pomo.

Amedai, katika tarehe hizo mahakama imepanga mawakili wa watetezi kumhoji maswali ya dodoso Mbatia kuhusu madai yake. Ni baada ya mwanasiasa huyo kuwasilisha mahakamani hapo nyaraka zake zinazothibitisha madai ya kuchafuliwa.

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi

Miongoni mwa madai ya Mbatia ni Selasini kumtuhumu kwa madai mbalimbali ikiwemo kwamba ni kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameuza shamba la NCCR-Mageuzi lenye hekari 56 , kufuja nyumba za chama hicho, ambapo amemtaka kwenda mahakamani kuzithibitisha na kama akishindwa kuthibitisha amlipe fidia.

Kwa upande wa vyombo vya habari vilivyoshtakiwa, vinadaiwa kuchapisha tuhuma zilizotolewa na Selasini dhidi ya Mbatia. Vyombo hivyo na Selasini kwa pamoja wanashtakiwa na Mbatia anyetaka walimpe fidia ya pamoja kiasi cha Sh. 10 bilioni kama wakishindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

Mbali na kesi hiyo iliyofunguliwa mahakama kuu, Mbatia amefungua kesi nyingine ya madai Na. 87/2023, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, dhidi ya Selasini, akitaka amlipe fidia ya kiasi cha Sh. 500 milioni, kwa madai amelichafua jina lake kwa kumtuhumu kuwa amewaomba rushwa ya Sh. 50 kila mmoja, waliokuwa wagombea viti maalum kupitia NCCR-Mageuzi, akiwemo Susan Masele.

Tayari mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, imetoa tangazo katika Gazeti la MwanaHALISI, ikimtaka Selasini ahudhurie kwenye usikilizwaji wa kesi hiyo tarehe 12 Julai 2023. Ni baada ya mwanasiasa huyo kudaiwa kukaidi wito wa awali wa kufika mahakamani Juni mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!