Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Wafanyabiashara Kariakoo waibua mapya, Lissu atoa kauli
Biashara

Wafanyabiashara Kariakoo waibua mapya, Lissu atoa kauli

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema alipotembelea sokoni Kariakoo
Spread the love

 

BAADHI ya wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, wamedai changamoto wanazokabiliana nazo zinasababishwa na masuala mbalimbali, ikiwemo kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Madai hayo yameibuliwa leo Jumatano, tarehe 5 Julai 2023, katika mkutano wa wafanyabiashara na Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani, Chadema, Tundu Lissu, uliolenga kuainisha changamoto wanazopitia.

Katibu Mkuu wa Jumuita ya Wafanyabiashara Kariakoo, Uroki Ombeni, amedai baadhi yao wanasakamwa kutokana na itikadi zao za kisiasa.

“Sheria za nchi zinasema kila mtu ana haki ya kuishi, kufanya jambo analotaka na kujiunga na chama anachotaka. Shida kubwa inayoikabili Kariakoo ni baada ya uchaguzi, kuna kundi linapita linaratibu watu, hutu alikuwa anashabikia kundi gani? Ndiyo maana unaona Kariakoo inasakamwa sababu ya itikadi za kisiasa,” amedai Ombeni.

Naye Venus Mrema, amedai changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa soko hilo ni kodi, akidai Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuwa ikiwakadiria kodi kubwa ulinganisha na uhalisia wa vipato vinavyotokana na biashara zao, pamoja na changamoto za mfumo wa forodha bandarini.

Katika hatua nyingine, Mrema ameitaka Serikali kuwadhibiti wafanyabiashara wa kigeni kutofanya biashara zinazoweza kufanywa na wazawa.

Aidha, Mrema ametahadharisha athari zitakazotokana na ujenzi wa mradi wa kituo cha biashara na logistiki cha Afrika Mashariki, unaofanywa Ubungo, akisema ukianza kufanya kazi utauwa baishara za wazawa.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo

“Huu ujenzi wa soko la Ubungo ndiyo msiba mkubwa, hakutakuwa na kitu cha kufanya sababu kama ninaenda China kuleta vitenge sasa watamleta mchina aje auze moja kwa moja. Huu mradi walitaka waupeleke Kenya wakakataliwa lakini sisi tunavyouruhusu tunauwa wazawa. Tunaomba Serikali ilinde wazawa,” amesema Mrema.

Akizungumza baada ya malalamiko hayo kuibuliwa, Lissu amedai chanzo chake ni Serikali kuweka kiwango kikubwa cha mapato bila kuangalia uhalisia wa mwenendo wa biashara na kipato chake.

“Wao wanapangiwa malengo na Serikali, TRA tunataka mwezi huu mtuletee trilioni 5 hapa mtaani mnaweza toa trilioni 5? na TRA isipofikisha lengo kamishna na watu wake hawana kazi. Malengo ndiyo yanaumiza watu sababu hayalingani na hali halisi ya biashara zetru na vipato vyetu na inakuwa hivyo sababu hatuna haki za walipa kodi,” amesema Lissu .

Amedai, baadhi ya watu wanalazimika kukwepa kodi ikiwemo kutumia mashine za EFD, kutokana na ukubwa wa viwango vyake.

“Watu hawahitaji kufukuzana na TRA kuhusu kutoa risiti, kwetu kwa nini tunafukuzana na TRA? Sababu ni ileile umelipia mzigo bei kubwa bandarini kuliko bei uliyonunua na ukiuza ukitoa risiti wanavyotaka hutafanya biashara, watu wanalazimika kuwa wakwepa kodi sababu ili biashara iende inabidi wakwepe wasipokwepa watafilisika,” amedai Lissu.

Aidha, ameshauri mifumo na sheria za kodi zirekebishwe ili viwango vya kodi viwe wazi, akidai hali ilivyo sasa inatokana na maamuzi ya TRA kuwapangia wafanyabaishara kodi inavyotaka.

“Tunahitaji kufanya mabadiliko ya mfumo wetu wa kodi, usiokuwa na haki kwa mlipa kodi. Tunahitaji kuwa na mfumo, sheria na mamlaka inayoongozwa na haki ya mlipa kodi ambazo TRA na maafisa wake hawawezi kujipangia kodi wanavyotaka. Tunataka sheria inayoweka viwango vya kodi,” amesema Lissu.

Kufuatia malalamiko hayo, MwanaHALISI Online, imemtafuta Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, kwa ajili ya ufafanuzi wake, ambaye amesema hawezi kuzungumzia sababu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameunda kamati maalum kwa ajili ya kuyasikiliza na kushauri namna ya kutatua.

“Sina coment, waziri mkuu aliunda kamati kushughulikia suala la Kariakoo nasubiri uamuzi wa kamati. Ripoti ikishafika kwa waziri mkuu atatoa maagizo namna ya kushughulikia,” amesema Kayombo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!