WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana mkoani Mtwara (Mtwara Girls High School), wameishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaondolea changamoto ya uhaba wa maji iliyodumu shuleni hapo kwa muda mrefu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).
Shukrani hizo zimetolewa na wanafunzi hao, baada ya huduma ya maji ya uhakika kurejea shuleni hapo kufuatia hatua ya Rais Samia kuzindua chujio la maji katika mradi wa Mangamba.
Sekondari ya Mtwara Girls ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huo uliozinduliwa rasmi na Rais Samia katika ziara yake ya kikazi kwenye mikoa ya kusini, aliyofanya hivi karibuni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Farida Twaha amesema “tunafurahia huu mradi mpya uliozinduliwa na Rais Samia, umesaidia kutatua changamoto ya maji iliyokuwepo muda mrefu. Kabla ya mradi kuzinduliwa kulikuwa na changamoto ya maji.”
Farida amesema, upatikanaji wa maji safi na salama utawasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku, kutokana na watoto wa kike kuwa na uhitaji mkubwa.
Leave a comment