December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtandao wa Elimu waweka wazi malengo yake

Spread the love

CLEMENT Maganga, Mwakilishi wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met), amesema kuwa mtandao wa elimu nchini imejiwekea malengo makuu matatu ya kuimarisha elimu. Anaripoti Danson Kaijage, Handeni … (endelea).

Kiongozi huyo akizungumza wananchi,wadau waelimu pamoja na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho wiki ya Elimu iliyofanyika kitaifa wilaya Handeni, Tanga, leo amesema kuwa malengo hayo matatu ni pamoja na kuongeza uelewa kwa umma juu ya haki elimu bora. 

Alitaja malengo mengine kuwa ni kuhamasisha serikali kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama wenye ulemavu, wito wa upatikanaji wa miundombinu na vifaa vya shule, mafunzo ya walimu ikiwa ni pamoja na walimu wenye ulemavu.

Maganga ameendelea kutaja malengo mengine ni kuhamasisha na kukumbusha jamii, Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuhusu umuhimu wa uwajibikaji wa pamoja katika masuala ya elimu na utekelezaji wa malengo endelevu la nne na la tano.

“Mkoa wa Tanga hasa wilaya ya Handeni kumechaguliwa kuwa sehemu ya kufanyia maadhimisho kutokana na juhudi zanazofanywa na wilaya hasa katika upande wa Elimu jumuishi,” alieleza Maganga.

Kwa upande wa baadhi wanafunzi wa kike walisema kuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali ya kukatisha masomo ikiwa ni pamoja na miundombinu kutokuwa rafiki.

https://www.youtube.com/watch?v=R-3zk5CjZ0U

Wakizungumza na waandishi wa habari wanafunzi hao wa kike walisema umbali wa kati ya shule na nyumbani unachangia zaidi wanafunzi wa kike kurubuniwa na waendesha pikipiki maarufu mama bodaboda.

Hadija Omari ambaye ni mwanafunzi wa kike alisema changamoto nyingine ambayo wanafunzi wanatukana nayo ni pamoja na ukata unaotokana na familia zao kwa familia kushindwa kuwapatia mahitaji wanayoyataka.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya Elimu Kitaifa wilayani Handeni alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa asasi zisizokuwa za kiserikali zinavyokuza na kuhamasisha umuhimu wa elimu na ubora wa Elimu nchini.

Shigella alisema kuwa pamoja na mambo mengine mkoa umejiwekea malengo ya kuifanya elimu kuwa shirikishi kwa jamii ili kuhamikisha inapandisha kiwango cha ufaulu.

error: Content is protected !!