April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema: Hatujui alipo Nyalandu

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema), kimeeleza kutojua alipo Lazaro Nyalandu, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Licha ya taarifa za kukamatwa kwake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Tumaini Makene, msemaji wa chama hicho amesema, taarifa za tukio hilo zipo ofsini kwake na kwamba, mpaka sasa hawajui alipo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Nyalandu ambaye alikuwa kada wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chadema Novemba 2017, alichukuliwa leo tarehe 26 Mei 2019 wakati akiwa kwenye kikao cha ndani cha chama hicho katika eneo la Itaja, Singida Kaskazini.

Makene amesema, wakati Nyalandu akiwa kwenye kikao hicho katika jimbo ambalo aliliongoza wakati akiwa CCM, walifika watu wenye silaha za moto waliojitamblisha kuwa ni askari, watu hao waliondoka na Nyalandu, David Jumbe na Mwenyekiti wa Chadema, Kata ya Itaja.

“Ni kweli mpaka sasa hatujui alipo, taarifa zilizopo mpaka sasa ni kwamba, watu hao waliofika eneo hilo na gari nyeupe, …walijitambulisha kuwa ni askari na walimuomba Nyalandu, Jumbe na mwenyekiti wa chama katika eneo hilo,” amesema Makene na kuongeza:

“Taarifa hizo ni kwamba, watu hao wakatoka nje na kuondoka nao. Hawakusema wanakwenda wapi. Naingia kwenye kikao kwa sasa, kama kuna zaidi nitumie ujumbe, nitakujibu.”

error: Content is protected !!