Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msuya awataka viongozi CCM kuisimamia serikali
Habari za Siasa

Msuya awataka viongozi CCM kuisimamia serikali

Hemed Msuya
Spread the love

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kilombero, wametakiwa kuisimamia serikali ili iendelee kutekeza ilani ya uchaguzi ya chama hicho ipasavyo. Anaripoti Victor Makinda, Morogoro … (endelea).

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kilombero,  Hemed Msuya, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwa ngazi ya wilaya  Kata ya Msolwa Steheni, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro jana.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM, Wilaya ya Kilombero, akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya chama hicho.

Msuya amesema CCM ndiyo chama kilichopata ridhaa ya wananchi ya kuunda serikali kupitia sanduku la kura, hivyo viongozi wa chama hicho wana dhima  ya kuwasimamia watendaji wa serikali na kuwawajibisha viongozi wote wanaoendekeza  urasimu na  ugoi goi katika kuwahudumia wananchi.

“Msiogope, chama ni zaidi ya serikali, kipo juu na serikali ipo chini ya chama. Mjitambue kuwa ninyi ni wasimamizi wa kuwasimamia viongozi wa serikali ili wafanye kazi kwa bidiii kutekeleza ilani ya CCM,” alisema Msuya.

Exif_JPEG_420

Aliongeza kusema kuwa CCM wilayani Kilombero, haitasita kuwachukulia hatua watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu  wao wa kuwahudumia wananchi.

Akizungumza kuhusu miaka 47 tangu kuzaliwa kwa CCM, Msuya amesema kuwa chama hicho kinajivuni misingi iliyoasisi na kuilinda, ikiwa ni uzalendo, utu, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ifakara Mji, wilaya ya Kilombero, Kasim Nakapala, akizungumza kwenye maazimisho hayo, alisema kuwa wakati tunasherehekea miaka 47 ya CCM, Halmashauri ya Kilombero imepokea miradi mingi ya maendeleo hivyo ni wajibu wa watendaji wote wa serikali kusimamia miradi hiyo ili ilete tija kwa wananchi.

“Tunaimshukuru serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea miradi mingi ya maendeleo wilayani kilombero, ikiwa ni miradi ya elimu, afya,kilimo, umeme na ujenzi wa barabara, hivyo watendaji wa serikali wanapaswa kuendana na kasi ya rais katika kusimamia miradi hiyo ili ituletee maendeleo,”alisema Nakapala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!