Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala
BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala

Spread the love

BENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu wa Shule za Msingi Mzambarauni na Uhuru Mchanganyiko na Sekondari za Pugu, Benjamin Mkapa na Jangwani, zilizo kwenye Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Walimu (TRC), Wilaya ya Ilala, kilicho jirani na Shule ya Msingi Uhuru Wasichana, ambako Meneja wa NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Edward Mpogolo.


Meneja wa NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Mhe. Edward Mpogolo vifaa saidizi kwa Walimu na Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule za Msingi Mzambarauni na Uhuru Mchanganyiko na Sekondari za Pugu, Benjamin Mkapa na Jangwani, zote za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, tukio lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Walimu (TRC), Wilaya ya Ilala. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Jiji la Dar es Salaam, Andrew Kihako na Afisa Elimu Jiji la Dar es Salaam, Musa Ally (wa kwanza kulia) wakishuhudia.

Vifaa saidizi vilivyotolewa na NMB kwa DC Mpogolo, ambaye naye alivikabidhi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu ni pamoja na fimbo nyeupe 60 kwa ajili ya wasioona, lensi 60 za kusomea kwa ajili ya wenye uoni hafifu, kofia 60 na mafuta ya kupakaa chupa 60 kwa ajili ya wenye ulemavu wa ngozi ‘albino.’

Akipokea msaada huo, DC Mpogolo aliishukuru NMB kwa sapoti kubwa inayotoa kwa Serikali kwenye Sekta za Elimu, Afya na Majanga na kwamba benki hiyo imethibitisha kwa vitendo ilivyo na moyo wa kujali jamii, bila kuyasahau makundi maalum ya wenye uhitaji.

Alibainisha kuwa, kupitia Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), NMB imejipambanua kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kufanikisha utoaji wa elimu bora mijini na vijijini na kuzitaka taasisi, mashirika, kampuni na wafanyabiashara kuiga mfano huo katika urejeshaji kwa jamii.

“Pongezi kwa NMB, kwa hakika mko ‘serious’ sana katika kutumia asilimia moja ya faida yenu kurejesha kwa jamii, ambako mmefanya mambo makubwa kote nchini kusaidia sekta za elimu na afya, huku mkiimbilia jamii ya wenye uhitaji wakati wa majanga.

“Leo mko hapa kukabidhi vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye uhitaji maalum kwenye shule zetu kadhaa, hiki mnachofanya ni miongoni mwa matendo ya huruma. Kwa niaba ya wanufaika wa msaada huu, nitumie nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza kwa matumisi sahihi ya Program ya Uwajibikaji kwa Jamii.

“Ndio maana naona mnastahili sio tu shukrani, bali pongezi kwa kazi kubwa mnayofanya kwa nchi yetu, kwa Serikali yetu, kwa wilaya yetu na kwa jamii yetu kwa ujumla. Ukitazama benki inayoongoza kwa gawio kubwa kwa Serikali ni NMB, benki inayotenga fungu kubwa la CSR ni NMB, hakika mnajali jamii,” alisisitiza Mpogolo.

Mkuu huyo wa wilaya akayataka mashirika, kampuni, taasisi na wafanyabiashara kuiga mwenendo wa NMB katika kutenga na kutumia ipasavyo fungu la CSR, huku akiitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuzibana taasisi zinazorejesha kwa jamii kwa maneno, huku pesa zao zikitumika nje ya urejeshaji kwa jamii.

Kwa upande wake, Prosper aliishukuru Serikali na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kuishirikisha NMB katika kufanikisha upatikanaji wa vifaa saidizi vya walemavu na kwamba changamoto zinazokwaza ustawi wa elimu na afya ni miongo ni mwa vipaumbele vya benki yake, kwani elimu na afya ni mtaji wa maendeleo ya Taifa.

“Tunanatmabua juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kusimamia upatikanaji wa elimu bora kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizi mijini na vijijini, nasi tukiwa wadau muhimu, tunao wajibu sio tu wa kuipongeza, bali kuiunga mkono kama hivi.

“Hivyo tuko hapa leo kukabidhi ‘Magnfier Lens’ 60 kusaidia wenye uoni hafifu, kofia 60 na chupa 60 za mafuta maalum ya kupakaa walemavu ngozi ‘sunscreen,’ fimbo nyeupe 60 kwa ajili ya wasioona, vifaa ambavyo tunaamini vinaenda kurahisisha ufundishaji na ufundishwaji wa walimu na wanafunzi wetu.

“Tunaishukuru CWT kwa kufikisha maombi yao kwetu, wakiamini na kutambua kwamba NMB ndio mahali sahihi pa kuelekeza changamoto zao nah ii inathibitisha namna mnavyothamini mchango wetu kwa jamii, ambako kwa miaka zaidi ya saba sasa tumekuwa tukisaidia kupitia asilimia moja ya faida yetu baada ya kodi,” alisema Prosper.

Awali, Katibu Mkuu wa CWT Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mahelela, alisema msaada uliotolewa na NMB ni matunda ya chama chake kupitia Kitengo cha Walimu Wenye Ulemavu, ambacho kilituma maombi hayo ya vifaa saidizi ili kurahisisha utendaji kazi wa walimu wake.

Aliishukuru NMB kwa kuyapokea maombi yao, kukubali kusaidia na hatimaye kutoa vifaa vilivyoombwa na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kubwa mno katika kuiunga mkono CWT na kuwasapoti walimu na wanafunzi wake, huku akiipongeza benki hiyo kwa kuwa kinara wa utambuzi na utatuzi wa changamoto za wenye uhitaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

error: Content is protected !!