Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wizara ya fedha yabanwa bungeni miradi ya fedha za UVIKO-19
Habari za Siasa

Wizara ya fedha yabanwa bungeni miradi ya fedha za UVIKO-19

Dk. Mwigulu
Spread the love

WIZARA ya Fedha, imebanwa bungeni jijini Dodoma, juu ya hatua ilizochukua kuhusu ubadhirifu uliojitokeza katika miradi iliyotekelezwa na fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kiasi cha Sh. 1.29 trilioni, ili kupunguza makali ya athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona ulioibuka 2019 (UVIKO-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Swali hilo limeulizwa na Mbunge Viti Maalum, Nusrat Hanje katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma, leo Jumanne.

“Taarifa ya CAG ya ufanisi ya 2021/22 inaonesha kwamba utekelezaji wa miradi inayodhaminiwa na UVIKO-19 hususan elimu na afya imekuwa inatekelezwa chini ya kiwango, tija ni kidogo sana na thamani ya fedha ni tofauti na kilichopo kwenye miradi. Nataka kujua serikali imejifunza nini na fedha za UVIKO sababu tunahitaji tuone thamani ya fedha na kilichopo kwenye mradi kinafanana,” amesema Hanje.

Baada ya Hanje kuuliza swali hilo, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, alimzuia Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, kulijibu akisema ni maoni ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aidha, Chande alisema Serikali inafuatilia kila siku miradi yote ambayo inafanyika nchini.

Awali akijibu swali la msingi la Hanje, lililohoji miradi iliyotekelezwa na fedha za UVIKO-19, Chande alisema katika sekta ya maji fedha hizo zimetumika kununua mitambo 25 ya kuchimba visima, seti tano za mitambo ya uchimbaji,  seti nne za vifaa vya uchunguzi wa maji chini ya ardhi, ujenzi wa mabwawa, pamoja na utekelezaji miradi ya maji 172 vijijini na 46 mijini.

Kwenye sekta ya elimu, Chande alisema fedha hizo zimetumika kujenga madarasa 12,000 katika shule za sekondari na 3,000 kwenye shule za msingi. Ukamilishaji wa vyuo vinne vya ufundi (VETA) ngazi ya mkoa na 23 ngazi ya wilaya.

“Kwenye sekta ya utalii imetumika katika ununuzi wa mitambo mitano ya ujenzi na ukarabati wa hifadhi 13 za taifa na kuimarisha mifumo ya utangazaji fursa za utalii. Katika sekta ya afya imetumika kununua X-Rays 169, C-T Scan 29 na MRI nne, mashine za huduma ya uchunguzi wa moyo saba, ujenzi wa nyumba 150 za wafanyakazi na uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo Sh. 5.42 bilioni zilitolewa kwa kaya masikini 51,290,” amesema Chande.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!