October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Msitu wa wanaCCM Nkenge haunitishi – ‘mgombea’ Chadema

Hilda Rweikila, aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum (Chadema)

Spread the love

JIMBO la Nkenge lililopo katika Wilaya ya Misenye, Kagera linawindwa na makada 19 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Danson Kaijage, Kagera … (endelea).

Mpaka sasa, Hilda Rweikila, aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum (Chadema), ndio mwanachama wa Chadema aliyejitosa kuwania jimbo hilo huku akisema, ‘CCM hawaaminiani, ndio maana kila mmoja analitaka jimbo.’

Balozi Dk. Diodorus Kamala, anayemaliza muda wake (CCM), ni miongoni mwa watia nia 20 kwenye jimbo hilo.

Hilda anatajwa kuwa na ushawishi kwenye jimbo hilo kutokana na uzoefu na umaarufu wake kisiasa.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Hilda amesema, amesukumwa kuchukua fomu ili ndoto ya wana Nkenge iliyoshindwa kufikiwa kwa miaka mitano iliyopita, aibebe kuelekea mafanikio hayo.

“Mimi sina kipato kikubwa lakini nina msimamo wa kuwatetea watu, na siyo kwamba sijatishwa kugombea, nimetishwa sana na wakati mwingine walikuwa hawanishirikishi vikao mbalimbali hasa vikao vya Kamati ya Fedha.

“…lakini nilikomaa nao, sikuogopa vitisho wala nini na ndiyo maana nimelazimika kuchukua fomu ili chama kikinipa ridhaa ya kugombea, niweze kupata uwanja mpana wa kuwatetea na kupeleka hoja zao bungeni,” anasema Hilda.

Anasema, tangu aanze kupiga kura, hajawahi kuipigia CCM na zaidi, wabunge wanaopatikana katika jimbo hilo, hawana msaada kwa wanachi.

Amesema, siasa ni mapambano hivyo hakuna sababu yoyote ya kuogopa kuwapambania watu ambao wanaohitaji mabadiliko.

Hilda akitumia msemo uliozoeleka kwa Wahaya kuwa waliohama wamekula “mandazi,” kwa maana ya kuhongwa anasema, watu wa aina hiyo ni wenye tamaa.

Awali, Jimbo la Nkenge liliwahi kuongozwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ambaye alishindwa na Dk. Kamala.

error: Content is protected !!