Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili ashangazwa Lissu kuibuka mkutano ACT-Wazalendo, Chadema yamjibu
Habari za SiasaTangulizi

Msajili ashangazwa Lissu kuibuka mkutano ACT-Wazalendo, Chadema yamjibu

Spread the love

OFISI ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, imeendelea kusisitiza vyama vya siasa kuzingatia sheria za nchi katika kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 huku akishangazwa kuona Tundu Lissu kuingia katika mkutano huo baada ya kufunguliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Hilo limesemwa na Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini humo, Sisty Nyahoza wakati akitoa salamu za ofisi ya msajili katika mkutano mkuu wa ACT-Wazaendo unaofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020.

Nyahonza amesema, uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa sheria hivyo vyama vya siasa vinapaswa kuzingatia sheria huku akiwaeleza kwamba zile barua ambazo zimekuwa zikiandikwa hazitakwisha.

“Zile barua zetu haziishi. Lengo ni kuhakikisha tunaendesha uchaguzi na usimamizi kwa mujibu wa sheria. Tusipozingatia sheria, hamuwezi kila chama kufikia malengo. Mko wengi na kila mmoja anataka kushinda,” amesema Nyahoza huku kelele zikiibuka ukumbini

Wakati kelele hizo zikiendelea, Nyahonza amesema, “fanyeni propaganda, mbwembwe zozote ikiwemo niliyoiona hapa ya mwalikwa kuingia kabla ya mkutano kufunguliwa, fanyeni tu, sisi tunawaasa, uchaguzi wote uende kwa mujibu wa sheria na sisi tutaendelea kusimamia sheria.”
Mwalikwa ambaye Nyahoza anamzungumzia ambaye ameingia ukumbini baada ya mkutano huo kufunguliwa na Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo ni Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema.

Lissu ameingia ukumbini wakati Maalim Seif amemaliza kufungua mkutano huo na ilikuwa zamu ya Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama kutoa hotuba yake ndipo Lissu akaingia ukumbini hali iliyoibua shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar, Salum Mwalimu alipotoa salamu za Chadema amemweleza msajili msaidizi, Nyahonza kwamba hawezi kuwapangia watu, “anataka kuwafundisha, nani aingie mwanzo na nani aingie mwisho, hayakuhusu Sisty, waachie wao, labda inakuuma kwa sababu jana ameteuliwa kwa kura nyingi. Nendeni mkawajulishe na wenzenu.”

Mwalimu ambaye ni mgombea mwenza wa urais Chadema, amemweleza Nyahonza na watumishi wengine wa umma ambao hawatendi haki, “anzeni kujiandaa, sisi tunasema tunashirikiana hatujasema tunaungana. Sasa anzeni kujiandaa.”

“Ukichukua ACT-Wazalendo na Chadema, sheria tunazijua, tena tunazijua kweli kweli,” amesema Mwalimu

Mwalimu amewatakia mkutano mwenza wajumbe wa mkutano huo huku akimalizika kwa kusema, “sisi Chadema tuko tayari kwa ushirikiano.”

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Bob Chacha Wangwe amesema, suala la sheria ni kwa vyama vyote “ufuatiaji wa sheria lazima ufanywe na watu wote. Sheria haipaswi kuwa na macho, iwe ni chama cha upinzani au CCM.”

“Uzoefu unaonyesha watumishi wa serikali hasa Sisty Nyahoza, Bunge na wengine wote wanafanya kazi zao kwa upendeleo kwa CCM. Niwakumbushe tu, fedha mnazopekea kama mishahra ni fedha za walipa kodi wa Tanzania, mnalinda mishahara ili kulinda vyeo vyenu lakini mnapaswa kulinda sheria zetu za nchi,” amesema Bob

Amesema, malengo ya Jukwaa la Katiba ni kuona utawala bora katika nchi, tungependa kuona ushindani mzuri hasa wa hoja.

“Tunakwenda katika uchaguzi, ningependa kuwasihi muweze kuungana na katika kuungana ni pale wote mkiwa na utawala wa kufanya hivyo. Mkiungana mafanikio yatakuwa makubwa zaidi,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!