HUMPREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukishughulikia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kunajisi Wimbo wa Taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Akizungumza na wanahabari leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020 jijini Dar es Salaam, Polepole amemtaka Jaji Francis Mutingi, Msajili wa Vyama vya Siasa kuchukua hatua dhidi ya chama hicho.
Polepole amesema, angetamani kuona Msajili wa Vyama vya Siasa anazungumza lugha ya kueleweka dhidi ya tuhuma hizo.
“Ningetamani msajili azungumze lugha ya kueleweka zaidi, watu wakikosea waaambiwe na sisi tukikosea tuambiwe, Wimbo wa Taifa unaunajisi halafu unatoka unasema wapi tumevunja sheria.

‘Wimbo huu sio wa CCM sio wa Freeman Mbowe (Mwenyekiti Chadema) na wenzake. Wimbo huu tunaimba tukiwa katikati ya vita tukiliombea Taifa,” amesema Polepole.
Aidha Polepole amekitaka Chadema kuwaomba radhi Watanzania kufuatia sakata hilo.
“Mimi nawaachia Watanzania, maana kabla hawajapewa nchi wanabadili wimbo wa Tanzania. Kabla hujaomba dhamana ya kuwa kiongozi wa nchi hii ushabadili wimbo wa Tanzania, unafanya wimbo wa chama chako.
“Mimi Watanzania naliacha hili kwenu, imetuuma sana tufanye siasa lakini tusitumie vitu vinavyogusa Watanzania vibaya bila aibu,” amesema Polepole.
Jana wakati akizungumza na wanahabari, Jaji Mutungi aliionya Chadema kutokiuka Katiba na Sheria za nchi kufuatia tuhuma hizo za kunajisi wimbo wa Taifa.
Wakati huo huo, Polepole amedai kuwa, kuna baadhi ya wanasiasa wakishirikishwa kwenye vikao vya NEC hukubali ajenda zinazoafikiwa, lakini wakitoka nje wanaeleza unafiki.
“Juzi tulikwenda kufuatilia maandalizi ya uchaguzi na yamekaa vizuri sana, tumepokea nyaraka na taarifa muhimu. Tulipewa kanuni za maadili ya uchaguzi, sheria iko vizuri asiwadanganye mtu. Tukikaa na tume tunazungumza lugha moja wakitoka nje wanaeleza unafiki,” amesema Polepole na kuongeza:
“Tukikaa na tume tunazungumza, tunasaini nyaraka wakitoka nje wenzetu wanasema tume hii mbovu. Huwa nawatazama. Kuna jamaa mmoja ambaye ni mbishi nasemaga huyu akitoka nje atakwenda kusema NEC si nzuri.”
Lissu aliyerejea nchini Tanzania tarehe 27 Julai 2020, akitokea Ubelgiji alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na risasi mjini Dodoma mwaka 2017, aliitaka NEC kutowaengua wagombea wa vyama vya upinzani.
Mmi nashauri sheria ichukuwe mkondo kwani kiasi gani wameonesha kuwa ni chama chenye mrengo wa kihuni ambao wakipewa dhamana hawatakawia kuiuza nchi
Wale askari magereza walioonyeshwa wanapandisha bendera za ccm nao wahojiwe na msajili