Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mrithi wa Maalim Seif aahidi haya
Habari za SiasaTangulizi

Mrithi wa Maalim Seif aahidi haya

Spread the love

 

OTHMAN Masoud Othman (58), Makamu wa Kwanza wa Rais Mteule visiwani Zanzibar, amewapa ahadi Wazanzibari. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Ahadi hiyo ameiweka kwenye andishi lake alilolitoa jana Jumatatu tarehe 1 Machi 2020, siku ambayo aliteuliwa na Rais wa Zanziba, Hussein Mwinyi kushika wadhifa huo.

Ni baada ya Maalim Seif Sharif Hamad (77), aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani humo, kufariki dunia tarehe 17 Februari 2021.

Andishi la Othman Masoud, alizaliwa 7 Februari 1963, Pandani, Wete- Pemba, aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, linasomeka kama ifuatavyo…

Ndugu zangu na wenzangu nyote, najua shauku na hamasa zenu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Najua imani yenu kwangu, hata wale waliokuwa wakihoji juu ya uwezo wangu au kufaa kwangu kwa nafasi hii walifanya hivyo kwa nia safi na hamu ya kupata mtu atayekidhi haja.

Hakuna anayeweza kukidhi vigezo wala viwango vya Maalim. Hakuna na hatotokea.

Mimi sikuwa nimeshindanishwa na yeyote bali nimetiwa katika mezani na kuonekana sio mzito zaidi, bali ninaelekea kwa yale viongozi wetu wa chama waliyoyaona yatafanana na uwezo wa kuendeleza msingi mzuri na madhubuti ambao mzee wetu Marehemu Maalim Seif kwa kushirikiana na Rais wetu Dokta Mwinyi wameujenga.

Kamwe sitojipima mezani ya Maalim daima sitotimia, bali nitajipima katika mezani ya matarajio ya watu wa Zanzibar na hatma ya nchi yao. Shauku na haki ya maendeleo. Haki ya maridhiano, utulivu na mshikamano.

Haki ya kuwa pale wanapostahiki. Haki ya kuwa na fahari na nchi yao. Hayo naamini yatapatikana kwa kumsaidia Rais wetu kujenga misingi imara ya taasisi za umma.

Misingi imara ya uwajibikaji na uadilifu. Misingi imara ya haki za kijamii. Misingi imara ya Sheria na usimamizi wa sheria na misingi imara ya uchumi kwa uwekezaji wa Serikali na ushiriki wenye tija wa sekta binafsi.

Zanzibar ina fursa ya kipekee kwa kutumia rasilimali watu, vipawa na uwezo wa watu wake waliopo ndani na nje. Kinachohitajika ni mashirikiano ya wote, mashirikiano ya dhati.

Sasa tunakwenda mbele kwa pamoja. Nawashukuru kwa namna ya kipekee.

Ahsanteni sana.
Othman M. Othman Shariff,
Makamu wa Kwanza Mteule wa Rais wa Zanzibar,
Jumatatu, Machi 01, 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!