May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaichapa Jkt, Yaisogelea Yanga

Kikosi cha Simba

Spread the love

 

USHINDI wa mabao matatu walioupata Simba dhidi ya JKT Tanzania, ulitosha kuwafanya kuibuka na pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kwa sasa Simba itakuwa inafikisha pointi 45, mara baada ya kucheza michezo 19, nyuma ya Yanga ambao wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 49 baada ya kucheza michezo 21.

Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yalifungwa na chriss Mugalu kwenye dakika ya  tisa ya mchezo na bao la pili likipachikwa na Luis Miquison dakika ya 38 na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Simba akiongoza kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kililejea kwa timu zote kushambuliana, huku Jkt wakionesha nia ya kutaka kuchomoa maboa haoyo dakika ya 90+6, John Bocco ambaye aliingia Uwanjani kuchukua nafasi ya Mugalu akapachika bao la tatu na kuifanya Simba kutoka kifua mbele kwenye mchezo huo kwa ushindi wa mabao 3-0.

Mara baada ya matokeo hayo Simba inatarajia kusafiri Siku ya kesho kuelekea nchini Sudan, kwenye mchezo wa michunao ya Ligi ya mabingwa dhidi ya El Merreikh ya Sudan, mchezo wa kundi A, utakaochezwa siku ya ijumaa tarehe 5 Machi 2021.

Simba mpaka sasa ndio vinara kwenye kundi hilo wakiwa na pointi sita mara baada ya kushinda michezo yao miwili ya awali ambapo alifanikiwa kushinda dhidi ya AS Vita ugenini nchini Congo DR na baadae kupata ushindi kwenye mchezo wa pili dhidi ya Al Ahly.

error: Content is protected !!