Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri
Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
Spread the love

 

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ajiuzulu kwa madai kuwa maagizo 12 aliyoyatoa mwaka 2023 kuhusu migogoro ya wananchi wanaoishi maeneo ya hifadhi za taifa, yamepuuzwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mpina ametoa wito huo leo tarehe 19 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma, akichangia mjadala wa bajeti pendekezwa ya Wizara ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, iliyowasilishwa na waziri wake, George Simbachawene.

Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amedai kumekuwa na changamoto ya watendaji wa Serikali kupuuza maagizo wanayopewa na viongozi wa ngazi za juu.

“Viongozi wetu sasa hivi wanapuuzwa, mfano mzuri Waziri Majaliwa aliwahi kuagiza maelekezo 12 kwa watendaji wa Serikali hasa wa uhifadhi, lakini mpaka nikaja hapa bungeni na vielelezo ikathibitika maelekezo ya waziri mkuu yamepuuzwa na yale matatizo yanaendelea mpaka sasa hivi,” amesema Mpina.

Mpina amesema “nilitegemea kwamba baada ya kupuuzwa maelekezo ya waziri, waliopuuza wangekuwa wamefukuzwa au waziri mkuu angekuwa ameshajiuzulu kwa sababu huwezi ukawa waziri mkuu halafu maelekezo yako yanapuuzwa.”

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Maelekezo yaliyotolewa na Waziri Majaliwa kuhusu migogoro hiyo, ni pamoja na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko yaliyotolewa taarifa bungeni na baadhi ya wabunge, juu ya tuhuma za wananchi kuteswa, kuumizwa na kuuawa kwa madai ya kuingia hifadhini kinyume cha sheria, ili waliohusika nayo waadhibiwe.

Maagizo mengine ni oparesheni za hifadhini zifanyike baada ya wananchi kushirikishwa na kupewa taarifa za kutosha badala ya kuwavizia. Mipaka ya hifadhi iwekwe nguzo ndefu zinazoonekana na mabango. Wahifadhi wawazuie wananchi kuingia ndani ya maeneo hayo, Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatilia malalamiko ya wananchi kuhusu baadhi ya wahifadhi kuingiza kwa makusudi mifugo hifadhini ili wapate fedha kupitia njia ya rushwa.

Maagizo mengine ni Sheria ya Uhifadhi Sura 282, ifanyiwe mapitio ili kuweka ulinganifu wa kiasi kinachopaswa kutozwa kama adhabu na kubainisha kiasi tajwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka utaratibu wa kisheria utakaolazimu mashauri ya mifugo kusikilizwa mapema na haraka, ili kukwepa gharama za utunzaji mifugo.

Katika hatua nyingine, Mpina ameshauri viongozi wa ngazi za juu za Serikali ikiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa wilaya, teuzi zao zifanyike kwa ushindani ili kupata wenye sifa stahiki.

“Teuzi za baadhi ya ajira kutolewa bila kufanyika ushindani kunatufanya kupata viongozi na watendaji dhaifu, ambao wanashindwa kutenda majukumu yao na kumpa kazi kubwa Rais. Kila leo kuteua na kutengua ni kazi kubwa pamoja na kusoma wasifu wa watu, wakati kazi hizi zingeweza kutangazwa watu wenye uwezo wakapata hizo kazi,” amesema Mpina.

Mpina amesema “kwa nini waziri leo ateuliwe, kwa nini asishindane tu kwenye interview?Kwa nini makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya wasishindanishwe maana tungeweza kupata wenye sifa.”

Kabla ya kumaliza kutoa maoni yake hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kilita Mkumbo, alisimama na kumpa taarifa akipinga pendekezo la Mpina la kutaka wateule kufanyiwa ushindani, akisema linakwenda kinyume na matakwa ya katiba yaliyompa mamlaka Rais kufanya uteuzi.

3 Comments

  • Nafikri Mh. Mpina aitake serikali ya CCM kuleta katiba ya Warioba, ambayo chama chake kiliikataa.
    Wataalam wapo wengi, lakin uteuzi unaangalia chama, Uwe mbunge n.k. wenye akili wengi hawako kwenye siasa za vyama.
    Katiba iliopo ndio inayompa rais NGUVU ya uteuzi.

  • Katiba siyo kitabu cha Dini kwamba kisibadilishwe Jamani, So Katiba iliandaliwa na binadamu hivyo hivyo binadamu anaweza kuifanyia changes endapo 1. Imepitwa na wakati. 2. Haikidhi na kufikia mahitaji ya watu n.k. mawazo ya mpina by the way yako sahihi kwa kuiweka serikali kuover see the ways forward for bring development.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!