CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa fedha za miradi inayoendelea kujengwa nchini, huku ikiiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), kuifuatilia kwa karibu ili kudhibiti uchotwaji wa fedha za umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana tarehe 18 Aprili 2024, mkoani Njombe, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emanuel Nchimbi, alisema wanaoliibia taifa ni sawa wanajiibia wenyewe na kukwamisha maendeleo ya taifa lao.
Dk. Nchimbi amewataka viongozi wa serikali kuwa na matumizi sahihi ya fedha za umma.
“Vyombo vyote vya Serikali vyenye mamlaka ya matumizi ya fedha za miradi, hakikisheni pesa hizo zinatumika kihalali na msisubiri kukamata walioiba bali ni lazima mdhibiti na kuzuia mianya ya uibaji,” alisema Dk. Nchimbi na kuongeza:
“TAKUKURU hakikisheni miradi yote hasa mikubwa ya maendeleo mnaifuatilia tangu ikiwa inaanza kuhakikisha hakuna fedha ya umma inaibiwa na kutumika vibaya, tunataka thamani ya fedha ieandane na thamani ya mradi husika. “
Leave a comment