Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mollel aomba dirisha maalum la Visa kwa wanafunzi kwenda kusoma China
Elimu

Mollel aomba dirisha maalum la Visa kwa wanafunzi kwenda kusoma China

Spread the love

MKURUGENZI wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, ameishukuru China kwa kufungua mipaka yake na ameomba Ubalozi wan chi hiyoo hapa nchini kufungua dirisha maalum kwa wanafunzi wanaoomba visa kwenda kusoma nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mollel amesema kuna idadi kubwa ya wanafunzi wa Tanzania ambao wangependa kwenda kusoma nchini China hivyo ameuomba ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini kufungua dirisha hilo ili wanafunzi wanaoomba Visa wapate kwa haraka na kwa wakati.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kuwaaga vijana 46 wa Tanzania wanaokwenda kusoma fani mbalimbali nchini China kwa ufadhili wa serikali ya nchi hiyo, fursa ambayo hutolewa kila mwaka.

Mollel alisema China ina vyuo vingi bora ambavyo vinatoza gharama za kawaida kumwezesha kila mtanzania anayetaka kwenda kusoma nchini humo kumudu gharama hizo za masomo.

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha na wageni waliohudhuria hafla ya kuwaaga vijana 46 wa Tanzania wanaokwenda kusoma fani mbalimbali nchini China kwa ufadhili wa serikali ya nchi hiyo, hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa China

“Kama mwanafunzi anataka kusoma vyuo vyenye mchanganyiko wa tamaduni, vyenye mahudhurio makubwa ya wahadhiri, vyenye usalama wa kutosha na gharama ndogo basi China ni chaguo bora kwa sababu haya yote yapo,” alisema Mollel

“Kwa hiyo wakati wowote serikali inapofikiria kuwapeleka wanafunzi nje ya nchi hata kupitia mpango wa ufadhili wa bodi ya mikopo, bajeti ile ile mnayowapa wanafunzi kwa vyuo vya Tanzania inaweza kukidhi gharama za vyuo vya China,” alisema

Mollel alisema kwa miaka mitatu mfululizo China ilikuwa imefunga mipaka yake hivyo wanafunzi kushindwa kwenda nchini humo lakini anashukuru kwamba hali imerejea kama kawaida na wanafunzi wa Tanzania wameanza kwenda nchini humo.

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, akijadiliana jambo na watu waliohudhuria hafla hiyo kwenye ubalozi wa China mwishoni mwa wiki.

Alisema wanafunzi wanapaswa kuripoti vyuoni mwezi Septemba hivyo aliomba ubalozi huo kuwapa upendeleo wa Visa za haraka haraka wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini humo.

“Tuwape fursa wanafunzi kufanya online booking mapema kwasababu tarehe 15 Septemba wanatakiwa kuripoti vyuni kwa hiyo wanatakiwa kupata kabla ya muda huo sasa tukiwacheleweshea wanaogopa kuomba vyuo vya China,” alisema

“Na hili linawezekana kwasababu Idara ya Visa imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa sana tunapokwenda kuomba Visa na hata sasa wanafunzi wangu wanaopitia Global Education Link kwa sasa wanoomba Visa hakuna anayekwama, tunapata ushirikiano mkubwa sana na msaada mkubwa,” alisema

Wageni mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye hafla ya kuwaaga vijana 46 wa Tanzania wanaokwenda kusoma fani mbalimbali nchini China kwa ufadhili wa serikali ya nchi hiyo, hafla iliyofanyika kwenye ubalozi wa China mwishoni mwa wiki.

“Lakini Booking ndiyo inachukua muda mrefu nawaomba mfungue dirisha maalum kwa wanafunzi wanapoomba Visa wawe wanapata kwa urahisi na kwa haraka tukiweza kufanya hili tutakuwa tumewamasisha wanafunzi wetu wengi kwenda kusoma China,” alisema Mollel

Alisema kutokana na uhusiano mwema uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na China, GEL itaendelea kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi wa Tanzania kwenda kusoma kwenye vyuo mbalimbali vya nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!