Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Biashara STAMICO yang’ara yabeba tuzo mbili
Biashara

STAMICO yang’ara yabeba tuzo mbili

Spread the love

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeng’ara katika kikao kazi cha Wenyeviti  na Watendaji wa Mashirika  ya Umma baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Taasisi za umma zilizofanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji na yenye tija kwa mwaka 2023. (Turn Around Company in Financial and Operational Performance as of June 2023). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia STAMICO imenyakua tuzo ya pili katika kundi la mashirika ya umma ambayo yametoa gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. (Outstanding Dividends payment SOE Category as of June 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dk. Venance Mwasse akiwa na tuzo hizo.

Tuzo hizo zimekabidhiwa leo jijini Arusha na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyefungua kikao kazi hicho na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk. Venance Mwasse pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya STAMICO, Meja Jenerali (Mstaafu) Michael Isamuhyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameipongeza STAMICO na kubainisha kuwa katika miaka miwili iliyopita ilikuwa inafikiriwa kufutwa kutokana na utegemezi lakini sasa  wameweza kuchangia hadi gawio kwenye mfuko mkuu wa Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Maisha ya kasino ni furaha, cheza Book of Eskimo kujichukulia utajiri 

Spread the love  KUPNGA ni kuchagua, chagua kuwa mshindi kila siku kupitia...

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

error: Content is protected !!