Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mmoja afariki, 13 wajeruhiwa vibaya Korea Kusini
Kimataifa

Mmoja afariki, 13 wajeruhiwa vibaya Korea Kusini

Spread the love

KIJANA mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 amewashambulia watu 14 kwa kuwagonga na gari na kuwachoma kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kusababishia kifo na majeraha katika jiji la Seongnam karibu na mji  mkuu Seol nchini Korea Kusini. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo … (endelea). 

Mshukiwa huyo aliendesha  gari lake hovyo na kuwagonga  watu watano, kisha alishuka na kuwachoma visu watu wengine tisa katika kituo cha ununuzi chenye shughuli nyingi ambapo mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 akifariki dunia baada ya shambulio hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo, wameeleza kuwa walimuona kijana huyo akiwa amevalia mavazi yote meusi pamoja na miwani nyeusi huku akiwa amebeba kisu mkononi mwake na ndicho alichotumia kuwashambulia wahanga baada ya kushuka kwenye gari.

“Ghafla, mtu mmoja alituambia kwamba mtu aliyetenda kosa alikuwa akija kwenye ghorofa ya pili, hivyo tukakimbia kwa hofu,” alieleza shuhuda wa shambulizi hilo huku akiongeza kuwa baada ya taarifa hiyo watu wengine walijificha katika jokofu kwa hofu.

Polisi wa eneo hilo walifanya jitihada na kufanikiwa kumkamata kijana huyo dakika 10 baada ya taarifa kusambazwa na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea. 

“Watu tisa walichomwa kisu katika eneo hilo, huku wengine watano wakijeruhiwa baada ya mshukiwa kuendesha gari kwenye njia ya watembea kwa miguu kabla ya shambulio la kisu”, alisema Lee Ki-in, afisa wa serikali ya Mkoa wa Gyeonggi, katika taarifa kwenye Facebook.

Majeruhi wa tukio hilo walikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ya haraka kwani wengi wa majeruhi walikuwa na hali mbaya.

Viongozi walijadili kuongeza doria za usiku katika maeneo ya starehe na mengine yenye watu wengi na kuimarisha ufuatiliaji wa kamera za usalama.

Mwezi uliopita, mtu aliyekuwa na visu aliwadunga kisu angalau watembea kwa miguu wanne kwenye barabara katika mji mkuu Seoul.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!