Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mzee amuangukia Majaliwa kutekwa kwa mwanaye, “bora nife”
Habari MchanganyikoTangulizi

Mzee amuangukia Majaliwa kutekwa kwa mwanaye, “bora nife”

Spread the love

KATIKA hali isiyo ya kawaida Mzee Isaac Mwasilu mkazi wa Kata ya Iyela – Mbeya Mjini mkoani Mbeya, amesema bora arudi nyumbani na kwenda kufa kama itashindikana kusaidiwa kupatikana kwa mtoto wake aliyepotea tangu tarehe 11 Novemba mwaka 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya …(endelea).

Ameda kuwa kwamba alichukuliwa kama ‘mateka’ na askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya aliyedaiwa kumtishia kuwa ‘atampoteza tarehe 10 Novemba 2021.

Akiomba msaada leo tarehe 3 Agosti 2023 mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema amehangaika juu ya kupatikana kwa mwanae kwa viongozi mbalimbali mkoani Mbeya, lakini hakuna msaada aliopata na hadi sasa hajulini kua mwanaye yupo hai au alifariki dunia.

Akisimulia mkasa huo, amesema mwanaye huyo huyo mwenye umri wa miaka 35 na watatu kuzaliwa kwa mara ya kwanza alikamatwa 1 Novemba 2013 askari ambao walienda kumkamata nyumbani kwake na kumpelekea kituo cha polisi kisha kurejea kuchukua gari ya mwanaye aina ya corolla.

Amesema baada ya kukamatwa, alifikishwa mahakamani na kubambikiwa kesi ya unyan’anyi.

“Walishindwa kupata ushahidi, mwanangu alikaa miaka miwili kisha ametoka mwaka 2015,” amesema.

Amesema baada ya kutoka hakurejeshwa gari lake lililokuwa linatumiwa na askari mmoja aliyemtaja kwa jina la Daniel.

Aidha, amesema tarehe 9 Disemba 2019 mwanaye huyo alikamatwa tena maeneo ya Southern sekondari na afande aliyemtaja kwa jina la Lumbamba.

Mzee huyo ameendelea kusimulia kuwa mwanaye huyo alipokamatwa alikuwa na kiasi cha Sh milioni 1.2 lakini alipofikishwa mahakamani na kubambikiwa kesi nyingine ya mauaji, afande huyo alimrudishia Sh 200,000 pekee.

Amesema kesi hiyo ilichukua miaka miwili hadi tarehe 16 Septemba 2021 alipoachiwa kwa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba mahabusu waliopo gerezani bila ushahidi waachiwe.

Mzee huyo amedai, tarehe 20 Oktoba alipoenda kudai gari pamoja na fedha milioni moja ambayo alinyang’anywa na askari, ndipo matatizo yalipoanza.

Amedai alimueleza Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya wakati huo, Ulrich Matei  na kutoa malalamiko yake.

Amedai baada ya malalamiko hayo ya kutaka kurejeshewa mali za mwanaye, ndipo tarehe 10 Novemba 2021 mwanaye huyo alipokutana na askari mmoja njia na kumueleza kuwa kwa kuwa ameenda kuwashtaki kwa bosi wao watampoteza.

Amesema kweli ilipofika tarehe 11 Novemba 2021 mwanaye huyo alipotea na mpaka sasa hajui alipo, kwamba amefariki au lah.

Baada ya kumsikikiza Mzee huyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wasaidizi wake kutoka ofisi yake kushughulikia suala hilo ili kupatiwa ufumbuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!