Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Rais Samia mgeni Rasmi Tamasha la Simba Day
Michezo

Rais Samia mgeni Rasmi Tamasha la Simba Day

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni Rasmi katika Tamasha la Michezo Simba Day litakalofanyika Jumapili ya tarehe 6 Agosti, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Isaya Temu, TURDARCo … (endelea).

Kupitia machapisho yao katika mitandao ya kijamii klabu ya Simba wameandika “Karibu kwenye kilele cha Wiki ya Simba. Karibu kwenye Simba Day, Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan (@SuluhuSamia). Hii ni siku muhimu kwa Klabu ya Simba na wapenda michezo wote nchini Tanzania.

Tunakushukuru na tanakukaribisha kwa furaha kubwa isiyo na kifani. Kwa kipekee kabisa, tunakushukuru sana kwa mchango wako mkubwa kwenye sekta ya Michezo na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Karibu sana Mheshimiwa Rais”.

Tarehe 06.08.2023 ni kilele cha wiki ya Simba Day na muendelezo wa matamasha yao ya kila mwaka ambayo hutumia kujumuika na washabiki wao, kutambulisha wachezaji wapya, benchi la ufundi, malengo na matarajio yao kuelekea msimu mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!