MKUTANO wa nane wa uhisani Afrika Mashariki (EAPC), unatarajiwa kuanza kufanyika tarehe 28 hadi 30 Juni 2023, visiwani Zanzibar.Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 27 Juni 2023 na Afisa Mtendaji Mkuu wa EAPC, Evans Okinyi, bodi za udhamini zinazofanya hisani, taasisi na mashirika yanayofanya kazi za kijamii pamoja na yanayotoa ruzuku kwa ajili ya miradi ya maendeleo Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, zitashiriki mkutano huo.
“Mkutano huu ni kwa ajili ya kuhamasisha suala la uhisani katika jamii na kujadili namna bora kuendeleza uhisani barani Afrika, kwa ajili ya kuleta maendeleo. Mkutano huo unaendeshwa na Mtandao wa Uhisani Afrika Mashariki (East Africa Philanthropy Network – EAPN), kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF),” imesema taarifa ya Okinyi.
Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 300, ambao watabadilishana uzoefu, kufanya tathimini ya pamoja na kuunda mipango ya kihisani na kijamii ili kuwekeza katika jamii barani Afrika.
Leave a comment