Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Milioni 250 za tozo zajenga kituo cha Afya Vumilia
AfyaHabari

Milioni 250 za tozo zajenga kituo cha Afya Vumilia

Spread the love

ZAIDI ya Sh milioni 250 zinazotokana na tozo za miamala ya simu nchini zimetumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya Vumilia kilichopo katika Kata ya Vumilia wilaya ya Urambo mkoani Tabora. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo imeelezwa kuwanufaisha wakazi wa Kata ya Vumilia ambao wamefafanua kuwa walikuwa wakitembea umbali wa kilomita 30 kwenda na kurudi kufuata huduma za matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Urambo.

Akizungumzia ujenzi huo Diwani kata hiyo, Usambile Kamuga (CCM) amesema wananchi walikuwa wanapata adha ya kutembea umbali mrefu kutoka eneo husika kwenda kufuata matibabu.

“Lakini pia kutokana na ujenzi huu, watu wamepata faida lukuki, mathalani mafundi wanaotumika katika ujenzi huu kati yao asilimia 70 wametoka kwenye kata yangu, ajira ndogondogo zimepatikana kwa vijana mbalimbali… wengine wanasogeza kokoto, wanabeba tofali, kiujumla mafundi wadowadogo wamefaidika sana na huu mradi.

“Haya yote ni matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imeamua kuwajengea watu wa Vumilia kituo cha afya katika eneo lao ikiwa ni sehemu ya mengi yanayofanyika katika wilaya ya Urambo,” amesema.

Mmoja wa wakaz wa Kata hiyo, Stela Kalembi amesema wanawake wamenufaika kupata huduma za matibabu karibu kwani walikuwa wanafuata huduma mbali.

“Tunashukuru sana Rais Samia ametuletea huduma karibu, tumuahidi kwamba tutautunza huu mradi kwa hali na mali kwa sababu hii ni faida kwetu sisi, tunamuombea aendelee kupiga kazi ili aweze kutuletea maendeleo zaidi,” amesema.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Louis Bura amesema sekta ya afya katika wilaya hiyo wamepokea Sh milioni 300 kwa ajili ya jengo la dharua katika hospitali ya wilaya.

“Nyingine tuliyopokea ni Sh milioni 250 fedha ambazo zimetokana na tozo za miamala ya simu. Fedha hizi zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya Vumilia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!