Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari DAWASA yafikisha maji Mongolandege, wananchi wapongeza
Habari

DAWASA yafikisha maji Mongolandege, wananchi wapongeza

Spread the love

 

WAKAZI wa Mongolandege wapatao takribani kaya 4,000 wameanza kunufaika na huduma ya majisafi kupitia mradi wa maji Mongolandege unaotekeleza na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mradi huo unaotekelezwa kwa kiasi cha Sh.700 milioni fedha za ndani umefikia asilimia 92 ya utekelezaji huku maeneo takribani yote yanayonufaika na mradi wakiwa wameanza kupata huduma.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kinyerezi Ndugu, Burton Mwalupaso alisema mradi unategemewa kukamilika kwa asilimia 100 ifikapo 30/6/2022 na wananchi wategemee huduma bora ya Majisafi.

“Kwasasa maeneo mengi wamekwisha anza kupata huduma ya majisafi, nawahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kuomba kupatiwa huduma, Mongolandege waliyasubiri maji kwa kipindi kirefu sasa yapo kwao ni fursa ya kila mmoja wao kupata huduma hii,” alisema Mwalupaso.

Mradi wa maji Mongolandege umehusisha kazi ya kuchimba na kulaza Bomba kubwa la inchi 8 na 6 Kwa umbali wa kilomita 6.9, pia kulaza mabomba ya usambazaji kwa wateja ya inchi 4,3,2 na 1.5 kwa umabli wa kilomita 16.6.

Naye Abuu Magaila, mwenyekiti wa mtaa wa Longani A, alisimulia jinsi gani wanapata ushirikiano kutoka DAWASA na wananchi kufurahia huduma ya majisafi.

“DAWASA wamekua karibu sana na wananchi, wamekua siku zote wasikivu na kujali kitu wananchi wanasema, kama Serikali ya Mtaa tuna furaha kufanya nao kazi, wananchi wangu sasa ni wenye furaha kwakua waliyangojea maji kwa muda mrefu na sasa wameyapata,” alisema Magaila.

Kwa upande wa wananchi, Rehema Kagambo mkazi wa Longani A, alisema wananchi walikua wakiyasubiri maji kwa muda mrefu na sasa wameyapata, huku akiwaomba wananchi wenzake kuendelea kujitokeza kupata huduma kutoka DAWASA kwani maji hayo ni ya nafuu sana na wote watayafurahia.

Mradi wa maji Mongolandege utahudumia wakazi wa Ulongoni A, Limbanga na Kibaha B huku kaya 4,000 zikinufaika na huduma ya majisafi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!