Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mei Mosi: Zitto apasuka
Habari za SiasaTangulizi

Mei Mosi: Zitto apasuka

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amepinga sababu zilizotolewa na Rais John Magufuli za kutopandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa miaka minne mfululizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 1 Mei 2019, jijini Dar es Saalam, Zitto amesema Serikali zote zilizopita zilifanya miradi ya maendeleo sambamba na kupandisha mishahara ya Wafanyakazi.

Zitto ametoa msimamo huo saa chache baada ya Rais Magufuli kueleza kwamba Serikali yake haipandishi mishahara ya watumishi wa umma kwa sababu inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, kwa minajili ya kumpunguzia mfanyakazi gharama za maisha.

Akihutubia wananchi katika maazimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ jijini Mbeya, Rais Magufuli amesema Serikali inakabiliwa na changamoto ya gharama za uendeshaji ikiwemo kulipa watumishi mishahara, deni la taifa, pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo. Na kuahidi kwamba miradi ya maendeleo ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi na kupunguza ukali wa gharama za maisha.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, amepinga sababu hizo huku akirejea Serikali za awamu zilizopita kwamba licha ya kutekeleza miradi ya maendeleo lakini zilikuwa zinapandisha madaraja, mishahara pamoja na kulipa stahiki za watumishi wa umma.

“Kwa nini Serikali isiwaambie ukweli wananchi kwamba imeshindwa kuongeza mshahara kwa sababu hali ya uchumi ni mbaya, gharama za uendeshaji serikali zimeongezeka na gharama ya kulipa deni la taifa imeongezeka badala ya kusingizia miradi?” Amehoji Zitto na kuongeza.

“Serikali hii ilikua ikiisema serikali ya awamu ya nne kulikuwa na ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma, vyeti feki pamoja na watumishi hewa na ukwepaji kodi, lakini serikali hiyo iliweza kupandisha mishahara kwa mujibu wa sheria. Alivyoingia madarakani Rais Magufuli aliondoa watumishi hao na kuzuia ufisadi, iweje ashindwe kuongeza mishahara?”

Zitto amesema nchi inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo bila kutumia maarifa na kujiandaa vyema, hali inayoathiri ukuaji wa pato la taifa na kupelekea Serikali kushindwa pandisha mishahara ya watumishi wake.

“Hapa kwetu tunatekeleza miradi mikubwa lakini pato la taifa linaporomoka kwa sababu tumetekeleza bila kutumia maarifa ya kutosha, malighafi za ndani zinazowezakana na kuandaa wananchi. Matokeo yake miradi badala ya kuchochea ukuaji wa uchumi, inasababisha uchumi kutokuwa kwa kasi,” amesema Zitto.

Aidha, Zitto ameishauri Serikali kuhakikisha kwamba shughuli za kiuchumi zinaimarika ikiwemo kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na ufanyaji biashara, ili kutengeneza fursa nyingi za ajira za kudumu na kuiwezesha serikali kupata mapato kupitia kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!