Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe kutumia mashahidi 26, vielelezo 34 kujitetea Machi 4
Habari za Siasa

Kina Mbowe kutumia mashahidi 26, vielelezo 34 kujitetea Machi 4

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na wenzake wakiwa mahakamani
Spread the love

 

UPANDE wa utetezi, katika kesi ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar ea Salaam, wanatarajia kutumia mashahidi 22 na vielelezo 24. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 24 Februari 2022 na mahakamani hapo, mbele ya Jaji Joachim Tiganga, na mawakili wa utetezi, baada ya washtakiwa kukutwa na kesi ya kujibu.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika keai hiyo ya uhujumu uchumi, namba 16/2021, ni waliokuwa makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Peter Kibatala, Wakili wa Mbowe, ambaye ni mshtakiwa wa nne katika keai hiyo, amedai mteja anatarajia kuita mahakamani hapo mashahidi 10 na kuleta vielelezo 20.

“Mshtakiwa wa nne atajitetea chini ya kiapo, anatarajia kuita mashahidi 10, plus yeye watakuwa 11 kwa ujumla na anatarajia kutumia vielelezo 20,” amedai Wakili Kibatala.

Naye Wakili wa mshtakiwa wa kwanza, Hassan, Jeremia Mtobesya, ameieleza mahakama hiyo kuwa, mteja wake anatarajia kujitetea kwa kuita mashahidi watano na kutoa vielelezo vitano.

“Mshtakiwa wa kwanza anategemea kuleta mashahidi watano, kwa hiyo na yeye atakuwa wa sita, atatoa vielelezo vitano kama sehemu ya utetezi wake,” amedai Wakili Mtobesya.

 

Kwa upande wake John Mallya, Wakili wa mshtakiwa wa pili, Kasekwa, amedai mteja wake anatarajia kuita mashahidi wawili na kutoa vielelezo vinne.

“Mshtakiwa wa pili amepanga kuleta vielelezo vinne kusapoti ushahidi wake na mashahidi wawili,” amedai Wakili Mallya.

Fredrick Kihwelo, Wakili wa mshtakiwa wa tatu, Ling’wenya, amedai mshtakiwa huyo anatarajia kuita mashahidi watano na kutoa vielelezo vitano.

“Kwa niaba ya mshtakiwa wa tatu sisi pia tumepokea maamuzi ya mahakama na mshtakiwa wa tatu atajitetea mwenyewe na atakuwa na mashahidi watano na vielelezo vitano.”

Makosa waliyokutwa na kesi ya kujibu pamoja na la kula njama za kutenda vitendo vya kigaidi, Kinyume na kifungu cha 4 (1 na 3 ), cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi namba 21 ya 2002, wanalodaiwa kufanya kati ya Mei Mosi hadi tarehe 5 Agosti 2020, katika Hoteli ya Aishi mkoani Kilimanjaro na maeneo mbalimbali yaliko jijini Dar es Salaam.

Wanadaiwa walikula njama za kutaka kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu katika maeneo ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, yakilenga kuleta hofu kwa Watanzania na kuleta madhara kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe na wenzake, pia walikutwa kesi ya kujibu katika shtaka la pili, la kula njama na kutenda kosa la kumjeruhi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kilimankaro, Lengai Ole Sabaya, lengo likiwa ni kuleta hofu kwa Watanzania na kutengeneza madhara kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Katika kosa hilo, wanadaiwa kukiuka kifungu cha 4 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Mbowe amekutwa na kesi ya kujibu katika shtaka la tatu la kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kigaidi, ambapo anadaiwa kukiuka kifungu cha 4 (1 na 3), cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Anadaiwa katika maeneo ya Dar es Salaam, Morogoro na Kilimanjaro, alitoa fedha kiasi cha Sh. 699,000 kwa washtakiwa wenzake, ilihali alijua zitatumika kama sehemu ya kuwapata wahusika kwa kutenda makosa ya kugaidi kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya waty, Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.

Katika shtaka la nne, la kushiriki vikao vya kupanga kutenda makosa ya ugaidi, washtakiwa wote walikutwa na kesi ya kujibu, ambapo wanadaiwa kukiuka kifungu cha 4 (1 na 3) na cha 5 (1), cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi na kifungu cha 57 (1) na 60 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Shtaka la mwisho, linamkabili mshtakiwa wa pili, Kasekwa, alikutwa na kesi ya kujibu, ambapo anadaiwa Bastola aina ya Luger A5340, aliyokamatwa nayo maeneo ya Rau Madukani, Moshi Kilimanjaro, tarehe 5 Agosti 2020.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 4 Machi 2022, ambapo wataanza kujitetea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!