Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the love

WAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewataka watanzania kuongeza jitihada za kuleta maendeleo pamoja na kukemea ubaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mbowe ametoa wito huo leo tarehe 9 Disemba 2023, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii. Tanganyika huadhimisha siku ya uhuru tarehe 9 Disemba kila mwaka.

“Tunapoadhimisha, naomba tujenge upya mioyo yetu na kuahidi kuwa jasiri tena katika harakati zetu za maendeleo na ustawi. Naomba tuwe hodari katika jitihada zetu za kujenga Tanzania inayojumuisha kila mmoja wetu bila ubaguzi, yenye haki kwa kila mmoja wetu, na yenye neema kwa wote,” ameandika Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema licha ya mafanikio mbalimbali ambayo Tanganyika imepata tangu uhuru, lakini bado inakabiliwa na janga la umasikini kwa watu wake.

“Tunaadhimisha miaka 62 ya uhuru tukikumbuka pia umasikini wa watu wetu katikati ya wingi wa rasilimali, fursa zilizopotea na ahadi zilizovunjwa kutokana na sera na uongozi ambao haukutumia nguvu na ujasiri wa Watanzania,” ameandika Mbowe.

Amewataka Watanzania waenzi juhudi za waliopigania uhuru kwa kulipigania taifa kwa ujasiri pamoja na kukataa ahadi alizoita za uongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

error: Content is protected !!