Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Mbappe na rekodi ya Dunia hii hapa
Michezo

Mbappe na rekodi ya Dunia hii hapa

Spread the love

 

JINA Kylian Mbappe sio geni kwa mwanasoka kindakindaki yani yule ambbae anapenda mpira sana. Mchezaji huyo alivuti wengi na anazidi kuvutia hasa vilabu vikubwa kama vile Real Madrid, Liverpool na vingine vingi kutokana na uwezo wake mkubwa alionao huku thamani yake ikizidi kuongezaka.

Alizaliwa nchini Ufaransa, huku baba yake akifahamika kwa jina la  Willfred Mbappe na mama yake Fayza Lamar. Ni mzaliwa wa jiji la Ufaransa ambapo alizaliwa na alikulia kijiji cha karibu kiitwacho Bondy, huku baba yake akiwa na asili ya nchi ya Cameroon yani bara la Afrika.

Kama wachezaji wengine walivyo na wakala tofauti na nje ya familia kwa Kylian ni tofauti ambapo yeye, baba yake ndiye wakala wake akiwa kama mchezaji, huku mama yake akiwa na asili ya Algeria. Mbappe ana mdogo wake anayefahamika kwa jina la Ethan Mbappe anayecheza katika klabu ya wado ya PSG, vilevile ana mdogo wake amabye wazazi wake walimuasili kwa jina anaitwa Jires Kembo Ekoko ambaye naye pia yupo kwenye soka.

Ukiachana na stori hiyo ya Mbappe, pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Alipokuwa mdogo Mbappe alijiunga na shule binafsi ya Kikatoliki huyo Bondy ambapo alichukuliwa kuwa mwenye vipawa vya kitaaluma lakini mkorofi. Alipofikisha miaka 15 alianza kusoma masomo ya Kihispania, na bahati nzuri akawa mzuri kwenye lugha hiyo.

Kadri siku zinavyokwenda Mbappe alianza kuwafuatilia kwa ukaribu wachezaji mpira maarufu kwa wakati huo na kuwapenda akiwemo Cristiano Ronaldo, Zinedine Zidane, Neymar, Lionel Messi, Ronaldinho, Ronaldo Nazario, Eden Hazard na Thierry Herny na wengine wengi. Hivyo basi akiwa mtoto aliweza kupokea jezi ya Robinho ya AC Milan kama zawadi kutoka kwa yaya wake ambao walikuwa wafuasi wa klabu hiyo ya Italia, lakini hata hivyo Mbappe alitamani kuichezea Real Madrid ya Uhispania.

Mbappé alifundishwa na baba yake, Wilfred, alipoanza soka na AS Bondy. Kocha wake mwingine alikuwa ni Antonio Riccardi ambapo alisema kuwa alifundisha vijana wengi lakini hakuwahi kuona kipaji kama cha mchezaji huyo.

Ndugu mteja usisahau kuwa meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Jisajili hapa.

Hatimaye, Mbappé alihamia akademi ya Clairefontaine, na kuonyesha kipaji chake kilichofanya kuvutiwa na wengie na kupelekea klabu nyingi za Ufaransa, na Real Madrid, Chelsea, Liverpool, Manchester City na Bayern Munich, kutaka kumsajili kumsajili. Akiwa na umri wa miaka 11, Real Madrid ilimwalika kufanya mazoezi na vijana wao wa chini ya miaka 12 na kutembelea vituo vya klabu.

Mnamo Julai 2013, akiwa na umri wa miaka 14, Mbappé alijiunga na akademi ya vijana ya Monaco, akitia saini kandarasi ya miaka mitatu. Klabu hiyo ilikuwa imeshinda ushindani kutoka kwa Real Madrid na Zinedine Zidane, ambaye alihusika sana katika juhudi za kumsajili kinda huyo.

Mnamo Oktoba 2015, Mbappé aliletwa na Leonardo Jardim kuwa mhimili mkuu katika timu ya akiba ya Monaco, lakini kiwango chake cha ustadi na ukomavu kilichochea kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa baada ya wiki tatu tu. Alianza kwa mara ya kwanza katika timu yake miezi miwili baadaye, tarehe 2 Desemba 2015, katika sare ya nyumbani ya 1-1 ya Ligue 1 dhidi ya Caen, akichukua nafasi ya Fábio Coentrão baada ya dakika 88.

Kwa hivyo Mbappé akawa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika kikosi cha kwanza cha Monaco, mwenye umri wa miaka 16 na siku 347, akivunja rekodi ya awali iliyowekwa na Thierry Henry mwaka wa 1994. Aliendelea kufanya vyema na Monaco na hatimaye kuendelea kuvutia vilabu vingi na vingi zaidi.

Mwaka 2017 alivunja rekodi ya uhamisho ambapo Paris Saint-Germain (PSG) ilitangaza kumtia saini Mbappé kutoka Monaco kwa mkopo na chaguo la lazima la ununuzi la Euro milioni 180 na kulingana na mkurugenzi msaidizi wa michezo wa PSG Luis Ferrer, mabadiliko katika uamuzi wa Mbappé kujiunga na klabu hiyo kwa kiasi fulani yalitokana na hotuba iliyotolewa na meneja Unai Emery nyumbani kwa kina Mbappé wakati wa kiangazi.

Ada ya Euro milioni 180 ilimfanya Mbappé kuwa kijana ghali zaidi kuwahi kutokea na mchezaji wa pili kwa bei ghali zaidi kuwahi (nyuma ya mchezaji mwenza Neymar), na kuvunja rekodi ya uhamisho mkubwa zaidi katika ligi ya ndani. Alikabidhiwa jezi nambari 29 alipofika katika mji mkuu wa Ufaransa.

Tarehe 8 Septemba 2017, Mbappé alicheza mechi yake ya kwanza ya PSG katika ushindi wa 5-1 wa Ligue 1 ugenini dhidi ya Metz, akifunga bao. Siku nne baadaye, alifunga bao lake la kwanza la Uropa kwa klabu katika ushindi wa 5-0 wa UEFA Champions League ugenini dhidi ya Celtic. Alionyesha nyota katika ushindi wa PSG wa 3-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa pili wa kundi la Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiwatengenezea mabao Edinson Cavani na Neymar.

Mnamo tarehe 6 Disemba, Mbappé alifunga bao lake la kumi la Ligi ya Mabingwa katika maisha yake ya soka katika kichapo cha 3-1 dhidi ya Bayern Munich, na kuwa mchezaji mdogo zaidi kufikia alama hiyo, akiwa na umri wa miaka 18 na miezi 11. Akiwa tayari ameshinda taji lake la kwanza la ligi akiwa na klabu, tarehe 8 Mei 2018, Mbappé alishiriki katika ushindi wa PSG wa 2-0 dhidi ya Les Herbiers katika fainali ya Coupe de France.

Mnamo Julai 2018, Mbappé alipewa jezi nambari 7 kwa msimu ujao akiwa na PSG, akichukua nambari ya kikosi iliyoachwa wazi na Lucas Moura.

Baada ya kuonekana anafanya vizuri sana Mwaka 2018 mwezi Mei Mbappe aliitwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kwaajili ya Kombe la Dunia la 2018 lililofanyika nchini Urusi, huku mnamo 21 Juni alifunga bao la kwanza la Kombe la Dunia katika ushindi wa 1-0 wa Ufaransa katika hatua ya makundi dhidi ya Peru.

Na hiyo ikamfanya kuwa mfungaji mdogo wa mabao zaidi Ufaransa katika historia ya Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 19. Mbappe alizidi kuweka historia ambapo mnamo tarehe 30 Juni 2018 alitajwa kuwa mchezaji bora w amechi katika ushindi 4-3 dhidi ya Argentina katika hatua ya 16 bora akiwa mefunga penati moja na kufunga mabao 2 katika mechi ya kombe la Dunia baada ya Pele kufanya hivyo mwaka 1958.

Mbappe alifunga mechi nyingi ikiwemo pia ya Fainali dhidi ya Croatia na kufanikiwa kuchukua Kombe la Dunia la Urusi huku akichukua tuzo mbalimbali ikiwemo ya kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.

Mbappe sasa ndiye nahodha w atimu ya Taifa ya Ufaransa baada ya kuchukua mikoba ya Huggo LLoris aliyesataafu.

Mbappe sasa yupo kwenye mahusiano na Ines Rau, mwanamitindo aliyebadili jinsia ambaye alipata umaarufu mwaka wa 2017, kama ilivyo kwa MARCA. Wawili hao walionekana pamoja kwa mara ya kwanza kwenye Tamasha la Filamu la Cannes mwezi Mei mwaka jana, na kuzua gumzo kuhusu uhusiano wa kimapenzi.

Licha ya kuwa na mafanikio mbalimbali Kylian Mbappe ahjawahi kushinda Kombe la UEFA barani Ulaya ambapo akiwa na timu yake ya PSG msimu wa 2019/20 waliingia fainali ambapo walimenyana dhidi ya Bayern Munich na wakapoteza.

Hivyo macho yao kwasasa yapo kwenye kombe hilo ambalo hawajawahi kubeba na wapo hatua ya 16 bora ambapo watakipiga dhidi ya Real Sociedad ya Hispania, huku timu hiyo ikitimua makocha mbalimbali kwa kukosa taji hilo kama vile Thomas Tuchel, Pochettino na wengine kibao na pia mpaka sasa ndio vinara wa LIGUE 1 wakiwa na pointi zao 40 kileleni.

Mbappe ameweza kutikisa dirisha la usajili kwa misimu miwili mfululizo ambapo vilabu vikubwa ikiwemo Real Madrid ilisadikika atahamia huko lakini mambo yaligonga mwamba kutokana na kiwango cha pesa ambacho PSG walimuwekea na kumpa majukumu makubwa klabuni ikiwemo yeye ndiye atachagua nani wa kuanza kwenye kikosi hicho au laa.

Lakini bado pia bado anahusishwa na klabu hiyo huku mchezaji huyo akiwa na ndoto ya kusaka mataji makubwa na tuzo kubwa pamoja na ile ya Ballon Dior. Lakini Rais ya klabu hiyo Nasser Al-Khelaif ambaye amezidi kusisitiza kuwa mbappe atasalia PSG ahataenda popote.

Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na kuwaniwa na vilabu vya EPL kama vile Arsenal, Liverpool, na nyingine kama vile Manchester United.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!