BARAZA la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura ya kziwekea vikwazo nchi za Urusi, Korea Kaskazini na Iran kutokana na kufanya makosa mbalimbali, anaandika Irene David.
Akizungumza na Baraza hilo, David Ciciline kutoka chama cha Demokratic amesema, Urusi inahitajika kuchukuliwa hatua kwa kosa la kuingilia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, sambamba na Korea Kaskazini na Iraq kuadhibiwa kwa kosa la kufanya majaribio ya makombora.
Shirika la ujasusi CIA ambalo limekuwa likichunguza kwa umakini uhusiano huu kati ya Marekani na Urusi, limebaini kuwa katika utawala wa Putin ulimsaidia Rais Donald Trump kumharibia sifa mpinzani wake, Hillary Clinton katika uchaguzi wa mwaka jana.
Rais wa Marekani Donald Trumph na timu yake wamekana kutohusishwa kwa Urusi na Rais wake Vladimir Putin, katika uchaguzi uliopita japo bado jambo hili linatiliwa mashaka.
Mpaka sasa bado polisi nchini Marekani chini ya Shirika la Ulinzi na Usalama (FBI) linaendelea kuchunguza kwa umakini suala hili.
Leave a comment