August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwakyembe awashukuru Watanzania

Spread the love

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe, amewashukuru viongozi mbalimbali wa serikali na Watanzania wote kwa ujumla waliohusika kufanikisha shughuli nzima ya kumpumzisha mke wake Linah Mwakyembe, anaandika Irene David.

Ametoa shukrani hizo kwa niaba ya familia yake na kuongeza kuwa Watanzania wote wanastahili pongezi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam leo, amesema kabla hajarejea ofisini kwake mjini Dodoma anawashukuru wananchi wote.

Shukrani hizo zimelenga Watanzania wote kwa ujumla wakiwepo wakazi wa Kyela alipozikwa mke wake, makanisa mbalimbali likiwemo kanisa la Moravian, Mashkeh akiwemo Mufti Mkuu na madaktari wote waliohusika kumsaidia marehemu.

Shukrani zingine alizitoa kwa wamiliki wa vyombo vya habari , watangazaji na waandishi wote wa habari waliofuatilia tangu ulipotokea msiba huo.

error: Content is protected !!