Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yaitaka Congo DR, Rwanda kuondoa majeshi mpakani
Kimataifa

Marekani yaitaka Congo DR, Rwanda kuondoa majeshi mpakani

Spread the love

WAKATI mahusiano ya kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda, ukiripotiwa kudorora, Marekani imezitaka serikali za mataifa hayo kuondoa majeshi yake mpakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Kwa mujibu wa Mtandao wa BBC Swahili, wito huo umetolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Anthony Blinken, alipozungumza kwa njia ya simu na Rais wa Congo, Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Katika hatua nyingine, waziri huyo wa Marekani alizitaka pande zote mbili kupunguza mvutano ili kuondoa mzozo wa kibinadamu katika mipaka kati ya mataifa hayo.

Rwanda na Congo kwa muda mrefu zimekuwa katika mgogoro ambapo chanzo kikidaiwa kuwa Rwanda inawaunga mkono wa taifa hilo.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Marekani, Matthew Miller, imesema “Blinken alitetea suluhu la kidiplomasia kwa mvutano kati ya nchi hizo mbili na akahimiza kila upande kuchukua hatua za kukomesha hali hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wanajeshi kwenye mpaka.”

Waasi wa M23, wanapigana mashariki mwa Congo, wamezidisha mashambulizi tangu mwezi uliopita, huku Umoja wa Mataifa ukiripoti kuwa watu wengine 200,000 wameyakimbia makazi yao.

Siku ya Jumatatu, ripoti zilisema mapigano makali yaliendelea, huku M23 wakichukua tena baadhi ya maeneo kilomita chache kutoka mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa DR Congo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza

Spread the loveWaziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu baada ya...

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

error: Content is protected !!