Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa G7 wajifungia kujadili vita ya Israel, Palestina
Kimataifa

G7 wajifungia kujadili vita ya Israel, Palestina

Spread the love

KUNDI la nchi saba zenye nguvu za kiviwanda duniani (G7), limejifungia nchini Japan kwa ajili ya kujadili vita kati ya Israel na Hamas, kundi la wanamgambo wa kiislamu linaloongoza ukanda wa Gaza, Palestina.Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 inayojumusiha nchi za Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani, pamoja na ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU),wamekutana katika kikao cha siku mbili kuanzia leo tarehe 7 hadi 8 Novemba 2023,Jijini Tokyo, nchini Japan.

Mkutano huo umeitishwa ikiwa vita hiyo imepigwa mfululizo wa siku 30, tangu Hamas wafanye shambulizi la kushtukiza upande wa Israel, Jumamosi ya tarehe 7 Oktoba mwaka huu, ambalo limepoteza maisha ya watu zaidi ya 1,400.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, mkutano huo wa G7 umeitishwa baada ya idadi ya mauaji ya raia wasiokuwa na hatia kuongezeka, pamoja na hofu ya kwamba vita hiyo inaweza kuenea hadi kufikia kuwa janga la kikanda.

Hadi sasa, watu zaidi ya 10,000 wameripotiwa kufariki dunia upande wa Gaza.

Mbali na vita ya Israel na Hamas, pia G7 itajadili vita kati ya Urusi na Ukraine, mahusiano yake na China na namna ya kuimarisha mahusiano na nchi za Asia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza

Spread the loveWaziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu baada ya...

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

error: Content is protected !!