December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mapigano  Israel, Gaza yaibuka tena

Spread the love
MASHAMBULIZI ya anga baina ya Jeshi la Israel na Wanamgambo wa Kipalestina ‘Hamas’, yameibuka tena baada ya kusitishwa wiki tatu zilizopita.Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa mitandao hiyo, Alfajiri ya leo Jumatato, tarehe 16 Juni 2021, Jeshi la Israel limeanzisha mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya kundi la wanamgambo wa Hamas,  katika Ukanda wa Gaza, likijibu mashambulizi ya kundi hilo.
Kundi la wanamgambo wa Hamas, lilirusha maputo ya moto kutoka katika Ukanda wa Gaza, kuelekea Israel, jana Jumanne tarehe 15 Juni 2021.
Kufuatia hatua hiyo, Jeshi la Israel lilitoa taarifa likisema, maputo hayo yalisababisha milipuko katika baadhi ya maeneo nchini humo.
Katika mashambulizi hayo, Jeshi la Israel limesema limerusha roketi zaidi ya 4,300, kuelekea eneo la wanamgambo hao, lililopo Ukanda wa Gaza na kuathiri sehemu zake 1,000.
Tarehe 21 Mei 2021, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) na kundi la Hamas,  ya lisitisha mapigano yaliyozuka tarehe 10 Mei mwaka huu, yaliyosababishwa na maandamano ya raia wa Palestina, ya kudai maeneo matakatifu kwenye Mji wa Al-Aqsa, ulioko Mashariki mwa Jerusalemu.
Mapigano hayo ya awali yalisababisha vifo vya watu 243, wakiwemo wanawake na watoto 100. Lakini yalisitishwa baada ya pande zote mbili kuwekwa chini na Jumuiya za Kimataifa, kwa ajili ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo wa muda mrefu.
Katika mgogoro huo, kundi la Hamas linashinikiza Israel iondoe Polisi wake katika maeneo hayo, likidai kuwa ni tishio kwa raia wa Palestina, likihofia raia hao kufukuzwa na walowezi wa Kiyahudi.
error: Content is protected !!