Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari kitaifa Miaka 60 ya Uhuru, wateja ZIC kupata ‘wese’ la kutosha
kitaifa

Miaka 60 ya Uhuru, wateja ZIC kupata ‘wese’ la kutosha

Maofisa wa Shirika la Bima Zanzibar wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji wa Shirika hilo, Mohammedi Ameir (wa pili kushoto) wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mipira maalumu iliyohifadhi namba tofauti za kiasi cha mafuta kitakachotolewa kwa washindi wa kampeni hiyo. Wengine ni Mkuu wa Kituo cha Mauzo ZIC tawi Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Amina Mohammed (kushoto), Ofisa uwekezaji na maendeleo ya Biashara ZIC, Rahim Hamza (Kulia) na Kaimu Meneja wa Tawi tawi ZIC Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Fatma Hadji (wa pili kulia)
Spread the love

Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limezindua kampeni yake kabambe inayoitwa “WESE NDIO MCHONGO” inayotoa fursa kwa wateja wake kote nchini kujaziwa mafuta kwenye vyombo vyao usafiri, ikiwa ni zawadi kwa wateja wa shirika hilo katika kuadhimisha ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya miezi mitatu uliofanyika jijini Dar es Salaam katikati ya wiki Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji wa Shirika hilo, Mohammedi Ameir alisema kampeni hiyo inawalenga wateja wa Bima Kubwa ya vyombo vya moto ambapo kila mteja ataekakata bima hiyo atakuwa kwenye nafasi ya kujipatia mafuta kwa ajili ya chombo chake cha usafiri.

“Shirika la Bima Zanzibar ni shirika ambalo linawateja wengi kutoka pande zote kwa maana ya Tanzania Bara na Zanzibar na siku zote tumekuwa karibu zaidi na wateja wetu. Kwa kuliona hilo tumeona katika kipindi hiki ambacho tunasherehekea maadhimisho haya muhimu kitaifa kwa pande zote mbili ni vema tuje na zawadi hii kwa wateja wetu.

“Pamoja na maadhimisho haya tunaamini washindi wetu wataweza kutumia zawadi hii ya mafuta kuokoa fedha ambayo wataitumia kwenye matumizi yao mengine ya mwisho wa mwaka ambao huwa unaambatana na sikukuu pamoja na mahitaji ya shule kwa watoto,’’ alisema.

 

Kaimu Meneja wa Tawi Shirika la Bima Zanzibar ZIC Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Fatma Hadji (wa pili kulia) wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mfano wa karatasi yenye namba inayoashiria kiasi cha mafuta kitakachotolewa kwa washindi wa kampeni ya “Wese Ndio Mchongo”. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji wa Shirika hilo, Mohammedi Ameir (wa pili kushoto), Mkuu wa Kituo cha Mauzo ZIC tawi Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Amina Mohammed (kushoto) na Ofisa uwekezaji na maendeleo ya Biashara ZIC, Rahim Hamza (kulia)

Akizungumza zaidi kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Kituo cha Mauzo ZIC tawi Posta Mpya jijini Dar es Salaam, Amina Mohammed alisema ili mteja aingie katika droo ya kujaziwa mafuta ni lazima afike katika ofisi za shirika hilo zilizopo kote nchini kwaajili ya kukata bima kubwa ambayo itamuwezesha yeye kupata bahati ya kujaziwa mafuta kuanzia lita tatu (3) hadi lita mia moja (100).’’

“Kitakachoamua kiasi cha mafuta anachostahili kupatiwa mteja ni bahati yake katika kuchagua kimpira kidogo (ball) chenye karatasi ndani iliyoandikwa kiasi cha mafuta aliyoshinda ili aweze kupatiwa mafuta yake kupitia vituo mbambalimbali vya mafuta kokote alipo nchini,’’ alisema.

Kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu, ikilenga kuwafikia wateja wote wa shirika la Bima Zanzibar waliopo Tanzania Nzima, ikiwa na kauli mbiu “Wese Ndio Mchongo, Kata Bima Tukajaze Wese”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudikakitaifa

Mondi abisha hodi tuzo za Grammy

Spread the loveMSANII wa Bongofleva, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka...

kitaifa

TIPER wataja dawa kudhibiti kupaa kwa bei za mafuta nchini

Spread the loveKAMPUNI ya Kuhifadhi Mafuta Tanzania (TIPER), imesema upo wezekano wa...

kitaifa

Kuelekea miaka 60 ya uhuru, GGML yaibuka mlipa kodi bora

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mine (GGML) imeibuka kuwa moja ya...

kitaifa

Serikali: Hakuna uhuru usio na mipaka

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania, imewakumbusha wananchi kuzingatia matakwa ya Ibara ya...

error: Content is protected !!