Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari kitaifa Kuelekea miaka 60 ya uhuru, GGML yaibuka mlipa kodi bora
kitaifa

Kuelekea miaka 60 ya uhuru, GGML yaibuka mlipa kodi bora

Spread the love

KAMPUNI ya Geita Gold Mine (GGML) imeibuka kuwa moja ya makampuni kinara kwa ulipaji kodi Tanzania kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Hayo yamebainishwa juzi Visiwani Zanzibar baada ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi kuitunuku cheti cha cha kutambua mchango wa GGML katika ulipaji kodi bora.

Rais Dk. Mwinyi alimkabidhi cheti hicho Makamu wa Rais wa GGML anayesimamia miradi endelevu, Simon Shayo hii ikiwa ni baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa pili kwa kulipa kodi ya zaidi ya Sh bilioni 338 kwa Serikali ya Tanzania.

Rais Dk. Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano la maonesho ya bidhaa za viwanda ambalo pia lilikuwa maalumu katika kujadili changamoto na mafanikio ya maendeleo ya uwekezaji kwa kipindi cha miaka 60 tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Awali Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Suzanne Ndomba- Doran amesema cheti ni ishara ya kutambua waajiri wanaounga mkono juhudi za serikali.

“Chama cha waajiri na ofisi ya waziri Mkuu uwekezaji, tunawapatia cheti waajiri ambao wanatoa ajira kwa wingi katika ajira za moja kwa moja lakini pia sio za moja kwa moja katika mnyororo wa thamani,” alisema.

Mbali na ulipaji wa mapato ya Serikali na uwekezaji kwenye jamii, Kampuni hiyo imetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 5,000 ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya kazi chini ya wakandarasi wa kampuni hiyo.

Aidha, hadi kufikia mwaka huu takriban asilimia 98 ya wafanyakazi wa GGML na asilimia 82 ya menejimenti ni Watanzania.

Malengo ya kampuni hiyo ni kuendelea kuwa mdau mwaminifu wa maendeleo kwa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa sehemu ya mustakabali wa kujenga uchumi wa viwanda na kufikia dira ya 2025 ambapo sekta ya madini imelengwa kuchangia walao 10% ya pato ghafi la taifa.

Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo GGML imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwani kwa kushirikiana na Serikali mkoani Geita imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia fedha za wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) zenye gharama zaidi ya Shilingi bilioni 36.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudikakitaifa

Mondi abisha hodi tuzo za Grammy

Spread the loveMSANII wa Bongofleva, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka...

kitaifa

TIPER wataja dawa kudhibiti kupaa kwa bei za mafuta nchini

Spread the loveKAMPUNI ya Kuhifadhi Mafuta Tanzania (TIPER), imesema upo wezekano wa...

kitaifa

Miaka 60 ya Uhuru, wateja ZIC kupata ‘wese’ la kutosha

Spread the loveShirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limezindua kampeni yake kabambe...

kitaifa

Serikali: Hakuna uhuru usio na mipaka

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania, imewakumbusha wananchi kuzingatia matakwa ya Ibara ya...

error: Content is protected !!