Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Majaji washauri vishawishi dhidi yao viondolewe
Tangulizi

Majaji washauri vishawishi dhidi yao viondolewe

Jaji Mstaafu, Profesa John Luhangisa
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, ameshauri kuwaondolea vishawishi majaji, ikiwemo kutowapa teuzi za nafasi za uongozi serikalini, ili watende majukumu yao kwa ufanisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo ulitolewa jana, tarehe 8 Desemba 2021, jijini Dar es Salaam, katika mdahalo wa kujadili hali ya haki za binadamu, ulioandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria, ikishirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Akizungumza katika mdahalo huo, Jaji Mstaafu, Profesa John Luhangisa alisema Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema kwamba, kazi ya ujaji ni wito na kuwa mazingira yao ya utendaji kazi lazima yaondolewe kwenye hali ya ushawishi.

“Mwalimu Nyerere alisema kuna kazi ambazo zinaweza zikafanywa na yeyote yule, lakini kuwa jaji au wakili sio mojapao ya hiyo kazi, akionesha umuhimu wa jaji na hakikmu ili tusilinganishe na yeyote yule,” alisema Prof. Luhangisa.

Prof. Luhangisa alisema “Mwalimu Nyerere ameeleza kwa kiasi gani zile kazi zinafanywa na watu very sensitive, inahitaji commitment (kujitolea) na mazingira wanayofanyia kazi yawaondoe katika hali ya kushawishia. alisema akijua utasimama kusikiliza kesi dhidi ya yeyote yule akiwemo rais.”

Prof. Luhangisa alishauri kipengele kilichopo katika Katiba kinachopendekeza baadhi ya nafasi wateuliwa majaji wastaafu kuzishika, ziondolewe ili wasitiwe majaribuni katika utendaji wao wa kazi.

“Mfano kuna nafasi katika katiba inayoelekeza nafasi maalum kwamba hii nafasi ya jaji mstaafu, hii mnaionaje kama sio kumuweka majaribuni? Unampa ushawishi fulani na mimi nitakapostaafu hii nafasi nifikiriwe kwenye uteuzi. Muwaache jaji wafanye kazi,” alisema Prof. Luhangisa.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Mstaafu Joaquine De Mello, alisema kuna tatizo kubwa la baadhi ya majaji na mahakimu kutozingatia viapo vyao kwenye utekelezaji majukumu yao ya kazi.

“Tuna shida kubwa kuhusu viapo, nadhani hatujui maana ya viapo na nimekaa mahakamani miaka 10 mashahidi wanaopoapishwa inakuwa formality, viongozi wananashinda Ikulu wanaapa, lakini tunajua tunaapa kwa ajili ya nini? Hatujui,” alisema Jaji De Mello.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!