January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia aruhusu mashabiki kuingia Bure, Tanzania dhidi ya Uganda

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameruhusu mashabki kuingia bure kwenye michezo miwili ya kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Uganda kwa timu za wanaume na wanawake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Michezo hiyo itapigwa hii leo tarehe 9 Disemba 2021, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 “Tanzanite” dhidi ya timu ya Taifa ya wanawake ya Uganda.

Mchezo wa pili ambao utapigwa majira ya saa 1:30 usiku utawakutanisha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambao watamenyana na timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes”

Samia ametoa ruhusa hiyo katikati ya sherehe ya maadhimisho ya maiaka 60 ya Uhuru, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyata na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Akiutangazia umma ulijitokeza uwanjani hapo, muongoza shughuli hiyo kupitia kipaza cha sauti alisema kuwa Rais ametoa ruhusa kwa michezi hiyo itakayochezwa baadae mashabiki kuingia bure.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kikiwa mazoezini

“Baadae kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu kati ya Tanzania na Uganda na Mheshimiwa Rais ametoa ruhusa kwa wananchi kuingia Bure.” Alisema mshereheshaji huyo

Vikosi vya vya timu ya Taifa ya Uganda tayari vimeshawasili nchini usiku wa kuamkia leo, majira ya saa 6 usiku tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki chini ya kocha wao Milsav Micho.

error: Content is protected !!