Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Yanga: Hatujakata tamaa na ubingwa
Habari MchanganyikoMichezo

Yanga: Hatujakata tamaa na ubingwa

Spread the love

KLABU ya Soka ya Yanga imesema haijakata tamaa na ubingwa Ligi Kuu Bara na hivyo wamesema kuwa watapambana mpaka dakika za mwisho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Maneno hayo yamesemwa leo na nahodha msaidizi Ramadhani Kabwili alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari, kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.

Kabwili amesema kuwa bado kama wachezaji wanamalengo ya kuchukua ubingwa, kwa kuwa hawapo mbali sana na vinara wa Ligi hiyo na hivyo alama tatu za mchezo wa kesho ni muhimu.

“Mchezo huo utakuwa mzuri, kwa kuwa bado tunamalengo ya kuchukua ubingwa, kwa kuwa hatuko mbali sana na wanaongoza Ligi, sisi wachezaji hatujakataa tamaa na molali ipo juu.” Alisema Kabwili.

Aidha Kabwili aliendelea kwa kusema kuwa wao kama Yanga, wanawaheshimu Ruvu Shooting kwa kiuwa inafundishwa na kocha mzuri.

Tunawaheshimu Ruvu Shooting, kwa sababu inafundishwa na kocha mzuri anayeijua Yanga, ila sisi tumejiandaa vizuri.” Aliongezea Mchezaji huyo

Kwa upande wa kocha wa makipa wa klabu hiyo Razak Siwa amesema kuwa, mapumziko ya wiki mbili yamewasaidia kujiandaa na michezo iliyobaki ya Ligi Kuu na hivyo wataanza na mchezo wa kesho kupata pointi tatu.

“Haya mapumziko sisi yametusaidia sana, na tumejiandaa kwa mchezo wa kesho na timu yote ipo vizuri.”Alisema Siwa

Yanga inaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 61, alama sita nyuma ya Simba wenye pointi 67.

Mpaka sasa Yanga wamebakisha michezo mitano kukamilisha Ligi Kuu kwa msimu huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yatoa msaada wa mil. 20 kwa waathirika mafuriko Hanang

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) sambamba na wafanyakazi wa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wadaka mirungi kwenye basi la Extra Luxury

Spread the loveJeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limekamata shehena ya dawa za...

Michezo

Vijana waadhimisha miaka 62 ya Uhuru kwa kushiriki michezo

Spread the loveUMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) tawi la Mlowo, jana...

Habari Mchanganyiko

Oryx yaungana na jamii kuwafariji waathirika maporomoko Hanang

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeungana na Watanzania kutoa pole...

error: Content is protected !!